Katibu wa Chama cha Walemavu wa ngozi(Albino) Mkoa wa Mbeya, William Simwali akizungumza na vyombo vya habari |
CHAMA
cha Walemavu wa Ngozi (Albino)Mkoa wa Mbeya kimesema matukio yanayoendelea ya
kukata viungo vyao pamoja na mauaji hayahusiani kabisa na masuala ya uchaguzi
bali ni imani za kishirikina zilizowatawala wananchi.
Hayo yalibainishwa
hivi karibuni na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya William Simwali kufuatia
kukatwa kiganja cha mkono wa kulia mtoto Baraka Cosmas(6) na watu wasiojulikana
na kasha kutokomea nacho kusikojulikana kijijini kwao Chipeta wilayani
Sumbawanga Mkoa wa Rukwa hivi karibuni na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa kanda ya
Mbeya.
Simwali
alisema watu wengi hivi sasa wanalinganisha matukio hayo na masuala ya uchaguzi
jambo ambalo sio la kweli kutokana na kushamili katika vipindi ambavyo hakuna
uchaguzi bali yanatokana na wakati ambapo Serikali na Taasisi mbali mbali kutoa
matamko ya kupinga mauaji ya Albino.
Alisema
mara ya kwanza matukio ya mauaji ya albino yalishamiri katika Kanda ya Ziwa
mwaka 2008 kipindi ambacho hakina uchaguzi wowote pamoja na Miaka mingine
iliyofuata ambapo aliitaka Serikali kufanya utafiti wa kina kubaini wahusika na
kuwachukulia hatua kali kama inavyofanya kwa majangili.
Alisema
matukio hayo Serikali inapaswa kulaumiwa kutokana na kutokuchukulia kwa umakini
katika kuyakomesha kama ilivyo kwa matukio mengine ambapo Serikali ikitoa muda
mambo hayo hutekelezwa ndani ya muda huo tofauti na ukomeshaji wa mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema
Rais alitoa aagizo la kuwaondoa majangili wanaoua tembo jambo ambalo lilifanikiwa
lakini pia agizo lake la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchi nzima
lilivyofanikiwa ndani ya muda mfupi hivyo kushangaza kushindwa kulitafutia
ufumbuzi suala la mauaji ya Albino.
Naye mweka
hazina wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Claud Mwakyoma alisema ili suala hilo
likomeshwe ni bora watu wenye ulemavu wakawekewa ulinzi maalumu ikiwa ni pamoja
na kutengewa eneo lao ili waangaliwe kwa ukaribu.
Alisema
kama suala la ulinzi litashindikana afadhali Albino wote wakakusanywa nchi
nzima na kupelekwa gerezani ili wakaishi kwa uhuru zaidi kutokana na kuwepo kwa
ulinzi kwa masaa 24 jambo ambalo litasaidia kukomesha vitendo hivyo kabisa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu.
Na Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment