Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 11, 2015

NEWS ALERT TUKIO KATIKA PICHA NA TAARIFA : WATU ZAIDI YA 30 WAHOFIWA KUFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOLIHUSISHA BASI LA ABIRIA LA MAJINJA NA LORI MAFINGA MAPEMA LEO.

Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lenye usajili wa namba T438 CDE lililolaliwa na Lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado. 

 Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.Hivi ndivyo Basi la Majanja linavyo onekana mara baada ya kuondoa Lori lilikuwa limekandamiza basi hilo.
 
 Umati wa watu mbalimbali wakiwemo wasafiri wasafiri waliokuwa katika mabasi mengine wakiwa wamejaa kushuhudia Ajali hiyo.
Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea

Muonekano wa Basi la Abiria na Lori yaliyo athirika kwa ajali hiyo 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA>>

No comments: