Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akihutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika Mtaa wa Kabwe kata ya Iyela Jijini Mbeya. |
Mratibu wa Kifua Kikuu Mkoa wa Mbeya akitoa neno la shukrani katika maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika Mtaa wa Kabwe kata ya Iyela Jijini Mbeya. |
Mkuu wa Wilaya pamoja na wageni wengine wakipokea maandamano |
Waandamanaji
katika maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa
katika Mtaa wa Kabwe kata ya Iyela Jijini Mbeya.
|
Kikundi
cha Kihumbe kikiongoza Maandamano.
|
Waandamanaji wakiwa na mabango katika maandamano ya siku ya Kifua kikuu
duniani.
|
Washiriki
katika maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa
katika Mtaa wa Kabwe kata ya Iyela Jijini Mbeya.
|
Washiriki
katika maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa
katika Mtaa wa Kabwe kata ya Iyela Jijini Mbeya.
|
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya imetajwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kifua kikuu katika
takwimu za Mkoa zilizofanyika Mwaka jana ikilinganishwa na Wilaya zingine.
Aidha
katika takwimu hizo zinaonesha jiji la Mbeya kuwa na wagonjwa wengi ambao ni 816
ikifuatiwa na Rungwe yenye wagonjwa 659,Chunya ni ya tatu ikiwa na wagonjwa
571,inafuatia Mbozi yenye wagonjwa 521,Mbarari wagonjwa 516,Kyela 313,Mbeya
vijijini 283 na ileje wagonjwa 72.
Hayo
yalibainishwa jana na Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Dk.Agnes Buchwa katika
maadhimisho ya Kifua kikuu duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika Stendi ya
Mabasi Kabwe jijini Mbeya.
Hata
hivyo mbali na Jiji la Mbeya kuongoza pia imeonekana ugonjwa huo kukua na
kuongezeka kila mwaka ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika miaka ya 2000.
Dk.
Buchwa aliongeza kuwa kwa sasa mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa mitano
nchini yenye wagonjwa wengi wa kifua kikuu.
Alisema
mkoani hapa wagonjwa wa kifua kikuu waliongezeka kutoka 3,743 mwaka 2000
hadi 3,952 mwaka 2005 lakini baada ya hapo wagonjwa walipungua hadi kufikia
2,949 mwaka 2008.
Alisema
baada ya hapo idadi ya wagonjwa imeabza kuongezeka tena ambapo mwaka 2009
wagonjwa walifikia 3,110,mwaka 2010 wakiafikia 3,215 na mwaka 2011 wakafikia
3,418 huku mwaka 2012 wagonjwa wakizidi kuongezeka na kufikia 3,502.
Alisema
takwimu za mwaka 2011 zinaoneshya kuwa katika kila watu 100,000 mkoani
Mbeya,watu 127 wana kifua kikuu na mwaka 2012 kati ya watu 100,000 watu 129
walipatikana na ugonjwa huo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa,ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao na wale
wanaobainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kuhakikisha wanafika katika
vituo vya afya husika kupata tiba kwakuwa huduma hizo hutolewa bure.
Aliongeza
kuwa Wananchi wanatakiwa kuhamamishwa na kufundishwa jinsi ya kujikinga na
maambukizi mapya ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuelezwa dalili zake ili kulinda
nguvu kazi ya taifa.
Katika
maadhimisho hayo Baadhi ya waathirika wa ugonjwa wa kifua kikuu waliotibiwa na
wanaoendelea kutibiwa walishauri wagonjwa wa ugonjwa huo kuzingatia masharti ya
tiba ili kuepukana na usugu wa ugonjwa unaoweza kuhatarisha zaidi maisha yao.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment