Wananchi walalamika kuwa wanataarifa kuwa Jiji walikataza kilimo hiki lakini watu wameendelea kulima
Wakazi wanaokaa Jirani na pembezoni mwa Mahindi hayo waingiwa hofu ya vibaka
Mahindi hayo yawa makazi ya Vibaka, Wavutabangi na waalifu wengine.
Haya ndiyo mahindi ambayo yapo Jirani kabisa na Mitambo ya Tanesco Sae Jijini Mbeya ambapo wakazi wamepata hofu kubwa kutokana na kutokuwa zao lakini Pori
Ingawa watoto wanapita hapa lakini ni eneo ambalo ni hatari
vijana wengi wacheza Kamari , wahuni wengine na wavuta Bangi wanashinda eneo hili la Sae Nyuma ya Mitambo ya Tanesco
Hapa sio salama
Hii njia zamani ilikuwa inapitika kwa Urahisi sana kwa sababu kulikuwa hakuna mahindi kabisa lakini sasa wakazi hawapiti kwa sababu ya haya mahindi hata mchana peupe watu hawapiti.
Bado haya ni matatizo sana eneo hili
Vibaka hukimbilia eneo hili
Makazi ya Vibaka
Je kwa Hali hii wananchi wataishi kwa amani... Huku jiji walikataza lakini iweje Mahindi haya yalimwe?
Moja ya Eneo Korofi Sae Jijini Mbeya ambapo watu wengi wamekuwa wakikabwa
Swali ni Je Jiji wameruhusu Shughuli za Kilimo cha Mahindi eneo la Jiji kama ilivyo Sae Mbeya? Je wananchi kama wanajua hawatakiwi kulima Mahindi haya kwa nini wameendelea kufanya hivyo? Hii ni sinto fahamu ambayo wakazi wa Eneo la Sae pia hawana majibu kwa kuwa wameendelea kupatwa na hofu kubwa kutokana na vitendo vya kuongezeka kwa wakabaji, wavuta Bangi, Wacheza kamali na makazi ya Vibaka.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment