Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 13, 2015

WASANII WAKUBWA WA FILAMU WATAKIWA KUWAINUA WASANII WACHANGA NA SIO KUWATOZA GHARAMA KUBWA.


Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Vanessa, Shukran Gidion akisalimiana na Msanii wa Filamu Charles Magari.


Mkurugenzi wa Vanessa Sekondari wakijadiliana jambo na msanii Mzee Magari.


Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Vanessa, Exon Mwakalikamo, akisalimiana na Mzee Magari.

Msanii mkongwe wa Filamu nchini, Charles Magari akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Shule ya Vanessa Sekondari.


.Mzee Magari na baadhi ya wasanii, waandaaji wa filamu na watengenezaji wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari Mbeya.

Magari akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

Mzee Magari akiwa na Mkurugenzi wa Vanessa pamoja na baadhi ya wasanii wakijadiliana jambo


Mwandaaji wa Filamu ya Black Valentine inayotaraijiwa kuzinduliwa, Yekonia Watson akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Mkuu wa Shule ya Vanessa Exon Mwakalikamo akielezea lengo la shule hiyo kushiriki katika filamu ya Black Valentine.
Baadhi ya Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakiendelea na majukumu yao ya kuchukua habari.
WASANII wakubwa wa Filamu nchini wametakiwa kuacha kuwatoza gharama kubwa wasanii wachanga pindi wanapokuwa wameombwa kushiriki katika moja za kazi zao.Rai hiyo imetolewa na msanii nguli wa Filamu nchini, Charles Magari maarufu kwa jina la Mzee Magari alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wake uliofanyika kwenye ofisi za shule ya Sekondari ya Vanessa iliyopo Isyesye jijini Mbeya.Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa taarifa kwa jamii kuhusiana na uzinduzi wa Filamu iitwayo Black Valentine inayotarajia kuzinduliwa kesho katika kilele cha siku ya wapendanao(Valentine day) uzinduzi utakaofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda sunset Soweto jijini Mbeya.Magari alisema mara nyingi wasanii wa Dar es salaam wamekuwa wakilalamikiwa na wasanii wa mikoani kuhusu kutoa majibu ya kukatisha tama pale wanapopigiwa simu wakiombwa kushiriki kwenye kazi zao sambamba na gharama kubwa  huku wakisahau kama nao walianza chini.Aliongeza kuwa pamoja na gharama kubwa wanazowatajia wasanii wachanga bado hucheza nafasi ndogo kwenye hizo kazi jambo ambalo huwakatisha tamaa watazamaji ambao wanakuwa na hamu ya kumuona msanii mkubwa jinsi alivyoshiriki.“ Mimi binafsi najivunia rekodi niliyonayo ambayo naamini hakuna msanii ambaye ameweza kuifikia kwani nimeshiriki katika Filamu kutoka Mikoa yote hapa nchini, gharama zangu ni nafuu kwani naelewana na mwandaaji pia napenda kucheza kuanzia scene tano kwenda mbele ili mashabiki wangu wafurahi uwepo wa mimi kwenye Filamu” alisema Mzee Magari.Aidha Magari aliwataka wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo kwani licha ya yeye kualikwa kama mgeni rasmi pia atatoa burudani kwa kutumbuiza nyimbo zake ambapo hadi sasa ana albamu moja yenye nyimbo 6 yenye jina la Dar raha.Kwa upande wake Mwandaaji wa Filamu ya Black Valentine, Yekonia Watson maarufu kwa jina la Aman, alisema watu wajitokeze kuangalia vipaji vya wasanii kutoka Mbeya walioshiriki katika Filamu hiyo sambamba na kujionea utofauti wa Valentine iliyozoeleka na iliyochezwa kwenye mkanda huo.Aidha alitoa wito kwa Wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuacha kushabikia kazi za wasanii kutoka nje ya mikoa yao kwa kuchangia na kuwaunga mkono wazawa kwa kununua kazi zao.Alisema katika filamu hiyo iliyotengenezwa na Enea Production imepata msukumo mkubwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Vanessa, Shukran Gidion, ambaye ameanzisha utaratibu wa kufundisha wanafunzi wake masomo ya   sanaa pamoja na kushiriki katika filamu hiyo.Mwisho.
Na Mbeya yetu

No comments: