Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 16, 2015

UZINDUZI WA FILAMU YA BLACK VALENTINE WAFANA NDANI YA UKUMBI WA MTENDA SUNSET MBEYA.

    Mgeni rasmi na baadhi ya wakurugenzi wakiwa wamekaa meza kuu wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa filamu ya Black Valentine.


   Mgeni Rasmi Charles Mwakipesile akikata utepe katika kasha la Cd  lenye filamu ya Black Valentine kuashiria  uzinduzi wa fialamu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya sherehe Esther Ngatian akiwatambulisha baadhi ya wageni waalikwa.

    Mkurugenzi wa Enea Production, Enea Mwalyaje(kulia) ambaye ndiye mtengenezaji wa Filamu ya Black Valentine akizungumza jambo.


Mkurugenzi wa Vanessa Sekondari, Shukrani Gidion(kulia) ambao ndiyo wadhamini wakuu wa filamu ya Black Valentine akiwasalimia wageni waalikwa.

   Mgeni rasmi Charles Mwakipesile akitoa hutoba baada ya kuzindua filamu ya black valentine.

   Mgeni rasmi akionesha Cd iliyozinduliwa.

Wasanii walioigiza katika filamu ya Black  Valentine wakiwa katika picha ya pamoja.


Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa filamu ya Black Valentine.Majaji wakifuatilia vipaji mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa vyuo walipokuwa wakishindana katika maonesho kwenye ukumbi wa Mtenda.


.Mzee Magari akishindana kusakata rhumba na mgeni rasmi Charles Mwakipesile.

HATIMAYE uzinduzi wa Filamu ya Black Valentine iliyoigizwa na wasanii kutoka jijini Mbeya imezinduliwa rasmi na kuingizwa sokoni.

Uzinduzi wa Filamu hiyo ulifanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset iliyopo Soweto jijini Mbeya ukisindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii nguli wa filamu na mziki wa taarabu kutoka Dar es salaam.

Wasanii hao ni pamoja na Charles Magari kutoka Bongo Movie, mwimbaji mahiri wa mziki wa taarabu Omari Tego sambamba na wasanii mbali mbali kutoka jijini Mbeya wakiongozwa na wanafunzi kutoka Vyuo vikuu vya Teku, Tia, Ilemi na Tumaini Makumira Mbeya.

Akizungumza katika sherehe hizo, Msanii Charles Magari aliwataka Wazazi  na walezi  kuvithamini vipaji vya vijana wao  hususani wanaoingia katika tasnia ya filamu kwa kuwaruhusu kwa kile kilichodaiwa ni sawa na kazi nyingine inayoweza kumuingizia kipato.

Magari alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi kuwakatalia watoto wao kujiunga na kazi ya sanaa kutokana na mtazamo hasi kwamba kazi ya sanaa ni ya kihuni jambo ambalo ni kinyume kabisa.

Alisema kazi ya sanaa husaidia kuleta ajira na kumuingizia kipato msanii kama zilivyo kazi zingine hivyo kuharibika kwa tabia ya mtoto kunatokana na malezi aliyoyapata tangu awali kutoka kwa wazazi wake.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo, Charles Mwakipesile, aliwapongeza wasanii kutoka Mkoa wa Mbeya kwa kuonesha vipaji na kuongeza kuwa eneo hilo linapaswa kuangaliwa na kuthaminiwa.

Alisema Mkoa wa Mbeya pekee unawasanii wengi lakini wameshindwa kuonesha uwezo wao kutokana na jamii kutowatia nguvu kwa kusaidia kununua kazi zao ili waweze kuinuka kiuchumi.

Mwakipesile alisema kazi ya sanaa kwa kiasi kikubwa imechangia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ambao kwa sasa wengi wao wamejikita kwenye filamu na mziki hivyo kutokuwa na vijana wanaozurura mitaani.

Aidha alimpongeza Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Vanessa iliyopo Isyesye jijini Mbeya, Shukrani Gidion, kwa kuanzisha utaratibu wa kufundisha sanaa kwa wanafunzi wake tangu wakiwa shule.

Alisema kitendo hicho alichokifanya Vanessa kinasaidia wahitimu baada ya kumaliza masomo kuwa na shughuli ya kufanya pamoja na kujitegemea kutokana na kuwa na ufahamu wa sanaa  alioupata akiwa shule.

Hata hivyo katika filamu ya Black Valentine asilimia kubwa ya wahusika ni wanafunzi na wahitimu wa shule ya Sekondari Vanessa.

Kwa upande wake Mwandaaji wa Filamu ya Black Valentine, Yekonia Watson maarufu kwa jina la Aman, alitoa wito kwa Wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuacha kushabikia kazi za wasanii kutoka nje ya mikoa yao

Alisema katika filamu hiyo iliyotengenezwa na Enea Production imebeba ujumbe mzito na unao eleza maana ya siku ya wapendanao na uvaaji wa nguo nyeusi tofauti na ilivyozoeleka kwa watu wengi kuvaa mavazi mekundu.

Mwisho.
 Na Mbeya yetu


No comments: