Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, February 24, 2015

SAFARI LAGER YATANGAZA BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI NYAMA CHOMA MBEYA 2015.


Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoliakizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akitangaza Bar zilizotinga fainali ya Safari lager nyama choma.

Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pichani.


Waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli

KAMPUNI  ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager  imetangaza bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano lauchomaji nyama Mkoani Mbeya lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.


Akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mikuyu, Meneja matukio wa Tbl Nyanda za juu Kusini, Abubakari Masoli alisema Bar zilizofanikiwa kutinga fainali zimepatikana kutokana na kura zilizopigwa na wateja wao.

Masoli  alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali kuwa ni pamoja na Karembo Bar iliyoko Sokomatola,New City Pub iliyopo Mwanjelwa,Tumaini Bar iliyopo Ilomba,Samaki Samaki Bar iliyopo Forest ya zamani na Nebana Bar iliyopo Soweto jijini Mbeya.

Alisema  fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya Februari 28,kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea zikisindikizwa na Bendi ya TOT, na  burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka Safari Lager.


Alisema shindano hili hufanyika kila mwaka,ambapo  kwa mwaka huu linafanyika kwa mara ya nane mfululizo  huku yakizinduliwa katika Mkoa wa Mbeya na kufuatiwa na mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na mwisho Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hilo limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.


“Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma”alisema Masoli na kuongeza.

“Tumezingatia maombi ya washiriki wa  mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”.

 Alisema  washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu ambazo ni  nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.


Alizitaja zawadi watakazopata washindi walioingia katika fainali na kuibuka na ushindi kuwa ni Mshindi wa kwanza ambaye ni Bingwa wa Mkoa atapata shilingi 1,000 000/=, Mshindi  wa pili shilingi 800,000/=,Mshindi wa tatu shilingi 600,000/=, mshindi wa nne 400,000/= na mshindi wa  tano 200,000/=.

Mwisho.

No comments: