Magari makubwa yakiwa yamesimama kusubiri miti kuondolewa barabarani katika eneo la Nanenane jijini Mbeya. |
Vibarua wakihangaika kuondoa miti iliyoangukia barabarani baada ya kuangusha mti katika shamba la Chuo cha Kiliomo Uyole. |
Baadhi ya Vibarua wakiwasaidia waliokata miti kuondoa barabarani ili kupisha magari kuendelea kupita. |
Barabara ikionekana kufungwa bila kuwepo kwa tahadhari yoyote. |
Miti ikiwa imeziba Barabara. |
Baadhi ya magari yakiwa kwenye foleni yakisubiri miti kuondolewa barabarani. |
MAGARI yanayotumia barabara kuu
ya TANZAM yamekwama kwa zaidi ya masaa
mawili katika eneo la Nanenane jijini Mbeya
baada ya mti mkubwa kuangushiwa barabarani.
Mti huo mkubwa umekatwa na watu
ambao hawakufahamika majina yao mapema ambapo walishindwa kuuzuia na kuangukua
kwenye barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hata hivyo watu hao hawakuweka
tahadhari ya aina yoyote wakati zoezi hilo likiendelea jambo lililosababisha
baadhi ya madereva wa magari madogo na magari ya abiria kulazimika kuchepuka na
kupita barabara zingine ili kuwahi muda.
Aidha hakuna Askari wa usalama
barabarani aliyeweza kugundua hali hiyo huku baadhi ya Madereva wa magari
makubwa wakilaani kitendo hicho kuwa ni kushindwa kuheshimu matumizi ya
barabara na watumiaji wengine.
Mwisho.
Na Mbeya yetu.
1 comment:
Uzembe usio na mantiki yoyote
Post a Comment