Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 19, 2015

KAMPUNI YA BIA TANZANIA(TBL) YAENDESHA SEMINA YA UCHOMAJI NYAMA MBEYA.


Chief Judge wa Safari lager Nyama choma, Manase Mwasha akiendelea kutoa mafunzo kwa washiriki wa semina elekezi.

Baadhi ya vifaa ambavyo mchoma nyama anapaswa kuwa navyo.

Chief Judge akionesha kibao kinachofaa wakati wa kutayarisha nyama.

Mkuu wa Matukio wa TBL Mbeya, Abubakari Masoli akieleza jambo.

Mratibu wa Safari lager nyama choma, Protas Singu akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina.


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakitunukiwa vyeti vya ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Matukio wa TBL Mbeya.





Washiriki wakifuatilia kwa makini mafundisho yanayoendelea.


Mmoja wa washiriki wa semina ya Safari lager nyama choma akichunguza kwa makini moja ya kifaa kinachotumika kupima joto la nyama.




KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager imetoa semina elekezi kwa Bar zaidi ya 20 zinazojihusisha na uchomaji nyama.

Semina hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa Shindano la kuipata bar inayoweza kuchoma nyama kuliko zote katika mkoa wa Mbeya maarufu kwa jina la Safari lager Nyama choma ambayo fainali yake inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya TIA Februari 28, mwaka huu.

Akitoa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa City pub Mwanjelwa jijini Mbeya, Jaji Mkuu (Chief Judge) Manase Mwasha, alisema Safari lager Nyama choma inapenda kutoa semina kwa washiriki kwa lengo la kuboresha majiko ya nyama choma.

Mwasha alisema majiko yakiboreshwa itakuwa rahisi kumridhisha mlaji ili aweze kupata nyama yenye ladha halisi na bora kwa mtumiaji na vile vile kumsaidia mchoma nyama aweze kupata kipato zaidi.

Alisema madhumuni ya safari lager nyama choma ni kuweza kuwaelimisha wananchi na wapenzi wote wa bia ya Safari na kuiwezesha jamii kufurahi zaidi chimbuko la safari lager.

Aidha Jaji huyo aliwakumbusha wachoma nyama kuhusu kuzingatia usafi kwa kuzingatia baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kuwa na nywele fupi na safi, kuvaa kofia au kitambaa kisafi cheupe, kuwa na kucha fupi na safi, kuvaa gloves wakati na kutayarisha nyama na uvaaji wa viatu vyeusi pamoja na Apron.

Mbali na kuwakumbusha kuhusu usafi binafsi pia aliwaasa kuweka mazingira safi yanayoizunguka biashara yake, vifaa vya kuchomea nyama, aina za nyama zinazostahili kuchomwa, utayarishaji wa nyama na uhifadhi wake.

Kwa upande wake Mkuu wa matukio wa TBL Mbeya, Abubakari Masoli alitoa wito kwa wafanyabiashara wa nyama choma kujitokeza kujaza fomu za Safari lager wezeshwa ili waweze kupatiwa ruzuku kwa ajili ya kuboresha biashara zao.

Naye Mratibu wa Safari lager Nyama choma, Protas Singu alisema baada ya semina hiyo kutakuwa na kampeni maalumu ya kuwahamasisha wananchi katika kila bar itakayoshiriki namna ya kuipigia kura ili iweze kuingia kwenye fainali.

Alisema bar zinazotakiwa kuingia fainali ni 5 tu hivyo wananchi watapaswa kuipigia kura baada ya kuridhishwa na huduma kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu ya mkononi.

“ Wananchi ndiyo wanaopaswa kuipigia kura bar itakayoweza kuingia fainali kupitia ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake kwa kufungua sehemu ya meseji anaandika neno safari kisha anaacha nafasi anataja Mkoa anaacha nafasi anamalizia na jina la Bar anayoipendekeza kisha anatuma kwenda namba 0653 215151” alifafanua.

Mwisho.

No comments: