Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 6, 2015

CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA KAMPASI YA MBEYA CHAJIVUNIA MAFANIKIO, CHA ONGEZA IDADI YA KUDAHILI WANAFUNZI.

Mkuu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya,Dionise Lwanga, akiwa ofisini kwake akiongea na Mwandishi wa Mbeya yetu blog


UONGOZI wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Mbeya umewashukuru wananchi kwa kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa mafanikio makubwa katika kipindi ambacho wanasherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.



Chuo hicho kinachomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda kilifungua tawi lake Mkoani Mbeya mwaka 2013 hivyo kupata mwitikio mkubwa katika kipindi kifupi.



Akizungumza na Mtandao wa Mbeya yetu blog, Mkuu wa Chuo hicho kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga alisema wakati tawi la Mbeya linafunguliwa lilikuwa linatoa wanafunzi katika ngazi ya Cheti lakini sasa kinatoa wahitimu wa Stashahada  ya kawaida(Diploma).



Lwanga alisema Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamekipokea Chuo hicho vizuri pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa kwani hadi sasa wananchi wa Kata ya Iganzo jijini Mbeya wamekipatia Chuo eneo la kujenga lenye ukubwa wa Heka 55.



Mkuu huyo wa Chuo aliongeza kuqwa mbali na kupatiwa eneo la kujenga Chuo pia kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na Kampasi ya Mbeya ambapo katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 kulikuwa na wanafunzi 44 na mwaka 2014/2015 chuo kina wanafunzi 165 kati yao 103 ngazi ya cheti na 62 wakichukua stashahada.



Alisema katika mwaka wa masomo 2015/2016 Chuo hicho kinauwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kutokana na kuendelea kuboresha mazingira na pamoja na upatikanaji wa nyumba za kulala wanafunzi wanaotoka mbali(hostel) ambazo ziko karibu kabisa na Chuo.



Lwanga alisema katika kusherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Chuo hicho kimeanzisha utaratibu wa kuwafundisha watumishi wanaojiandaa kustaafu, kutoa masomo ya ujasiliamali kwa wafanyabiashara na vikundi vinavyojihusisha na ujasiliamali elimu ambayo hutolewa bure na uongozi wa Chuo unaweza kuwafuata popote ingawa hutoa masomo katika muda wa jioni na muda wa kawaida(Full time).



Alisema kwa mwaka wa masomo 2015/2016 Chuo kimeanza kutoa nafasi za kujinga ambapo masomo yanatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu kwa wanafunzi wenye sifa wanatakiwa kuwahi mapema.



Mwisho.

Na Mbeya yetu



No comments: