Aidha
imeelezwa kuwa wadau wa sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo ni
utekelezaji wa adhma ya Serikali ya uanzishwaji wa mfumo shirikishi baina ya
serikali na sekta binafsi(PPP).
Wito
huo ulitolewa hivi karibuni na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina,
alipokuwa akipokea msaada wa magodoro kwa ajili ya kulalia wagonjwa kutoka
Benki ya NMB Kanda ya Mbeya.
Dk.
Mhina alisema wadau zaidi wanatakiwa kujitokeza kuchangia ukarabati na
maboresho ya Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ili iweze kutoa huduma kwa wananchi kwa
kiwango sahihi na kwa wakati muafaka baada ya miundombinu muhimu kukamilika.
Alisema
kutokana na msaada wa magodoro 17 uliotolewa na wafanyakazi wa Benki ya Nmb,
hivyo uongozi wa Hospitali unapaswa kutoa kipaumbele cha matibabu kwa
watumishi wa benki hiyo kwa kuwekewa mfumo maalumu utakaowawezesha kutopanga
foleni kusubiri matibabu.
“Labda
ni waagize watumishi wenzagu kuanzia leo watumishi wa Nmb wakifika Hospitalini
hapa kwa lengo la kutibiwa wapewe kipaumbele ikiwezekana wakaingizwa kwenye
mfumo wanaotibiwa wagonjwa wa bima ya afya” alisema Dk. Mhina.
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Glori Mbwile, akitoa shukrani
kwa msaada wa magodoro alisema bado kunachangamoto ya ujenzi wa njia za
kupitishia wagonjwa pamoja na kununulia vifaa katika Wodi ya watoto.
Alisema
wodi mpya ya watoto inahitajika kuwa na vitanda 80,magodoro na vifaa vingine
vinavyopaswa kuwemo wodini vyenye thamani ya shilingi Milioni 160 hivyo msaada
zaidi wa wadau unahitajika ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Awali
akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa magodoro, Meneja wa Kanda wa Benki ya
NMB, Lecrisia Makiriye, alisema mara nyingi benki huangalia maeneo ambayo
wateja wake wanapatikana kama katika sekta za elimu na afya ili kusaidia kupunguza
changamoto zinazokuwepo.
Alisema
Wafanyakazi wa Benki waliamua kuchangishana na kununua magodoro 17 pamoja na
fedha taslimu shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa njia za
kupitishia wagonjwa.
“Tunawiwa
kuona taasisi zinazohudumia umma tunazichangia ili kupunguza changamoto kwa
kuisadia Serikali ndiyo maana tukanunua magodoro haya machache ingawa tunaona
bado hayajamaliza tatizo pamoja na fedha za kujengea njia za kupitishia
wagonjwa” alisema Meneja huyo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment