Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 30, 2015

TRA MBEYA WAWEKWA KITIMOTO NA WAFANYABIASHARA, WASHINDWA KUTOA MAJIBU WAKATAA KULIPA ONGEZEKO LA KODI

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya ndg. Charles W. Sionga akitoa maelezo ya maelezo kuhusiana na kikap hicho na TRA

Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Anniny Lema, akiongea na wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya

WAFANYABIASHARA  wa Jiji la Mbeya wakiwa makini kuwasikiliza watumishi wa TRA MbeyaMchungaji Enock Mwandandila, alisema ongezeko la kodi halikuakisi hali halisi ya biashara na vipato vya wafanyabiashara na kutaka watunga sera kuangalia upya suala hilo kwani linaweza kuleta vurugu na kusababisha machafuko nchini.


WAFANYABIASHARA  wa Jiji la Mbeya  walifunga maduka yao wakipinga kulipa  mabadiliko ya sheria ya kodi ya 2014, ambayo walidai kuwa imeongeza ututiri wa kodi na kuendelea kuwakamua.


Wakizungumza baada ya kukutana katika mkutano wao uliofanyika ndani ya ukumbi wa Mkapa, Jijini hapa, ulioshirikisha watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Mbeya na jeshi la polisi, wafanyabiashara hao walisema kodi hiyo hailipiki na hawako tayari kulipa.

Awali baadhi ya wafanyabiashara walitoa malalamiko yao mbalimbali kuhusu suaala la sheria mpya ya kodi ya mwaka 2014 kuwa inaongeza kero kubwa kwa wafanyabiashara na itasababisha kukwamisha ustawi wao.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Masaga Salum, alisema mabadiliko hayo ya sheria ya kodi hayawatendei haki wafanyabiashara kwa kuwa hawakushirikishwa katika mchakato wa  kuandaliwa kwa sheria hiyo.

“Haiwezekani serikali ikawa inatoa misamaha ya kodi  kwa wawekezaji wakubwa toka nje ya nchi , huku ikitumia nguvu kubwa ya ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wadogo wa hapa nchini ambao ndio wapiga kura wanaowaweka madarakani ”

Mfanyabiashara mwingine, Tekla Mushi, alisema mbali na sheria mpya kuongeza viwango vya kodi mara mbili, lakini pia bado kumekuwa na mlundikano wa kodi kwa wafanyabiashara .

Alitaja baadhi ya kodi hizo ambazo alidai kuwa zinakwamisha ustawi wa wafanyabiashara kuwa ni kodi ya zimamoto, taka, Kosota, Leseni, pamoja na ushuru wa  Halmashauri na Mabango ya biashara.

“Mwenyekiti tulitaka pia ufafanuzi juu ya  TRA kutulazimisha wafanyabiasha kuonesha mikataba ya kodi za nyumba na mara baada ya kuonyesha hutukadilia kodi badala ya kumbana mwenye nyumba” alisisitiza Mushi.

Mchungaji Enock Mwandandila, alisema ongezeko la kodi halikuakisi hali halisi ya biashara na vipato vya wafanyabiashara na kutaka watunga sera kuangalia upya suala hilo kwani linaweza kuleta vurugu na kusababisha machafuko nchini.

“Serikali inapaswa kutambua kuwa  wafanyabiashara hawana kinua mgongo pindi umri wa kufanyakazi unapofikia ukomo, hivyo ongezeko la kodi hiliwezi kutekelezeka na tunaomba iundwe tume ya maridhiano ili kufikia muafaka”.

Hata hivyo, akijibu hoja za wafanyabiashara hao, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Anniny Lema, alisema suala la ulipaji kodi ni la kisheria na kwamba lawama kwa Mamlaka hiyo ni sehemu ya changamoto.

“Sisi ni daraja tu kati yenu na serikali, kikubwa mmetoa maoni yenu, kikubwa tutayafikisha sehemu husika na kama kutahitajika marekebisho wao ndio wenye uwezo wa kufanya hivyo” alisema Lema.

Kaimu Meneja huyo, alidai kuwa kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2014 viwango vya ulipaji kodi kwa wafanyabiadhara wadogo vimeongezeka  zaidi  ya viwango vilivyokuwepo mwaka 2013/14.

Alisema kuwa kwa wafanyabiashara wanaofikia makisio yanayozidi sh. Mil 4 hadi Mil 7.5 zamani walikuwa wakilipa shilingi laki moja kwa mwaka na sasa watalazimika kulipa shilingi laki mbili.

Mwisho.
Na Mbeya yetu 

No comments: