Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 16, 2014

WATANO WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 36 KUJERUHIWAVIBAYA WAKISAFIRISHA MAITI MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,


Waliofariki katika ajali ya gari iliyokuwa ikisafirisha maiti na kupinduka kisha kusababisha vifo vya watu watano wamefahamika majina yao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha kujulikana kwa majina hayo na kuwataja kuwa ni wanawake watatu na wanaume wawili ambao ni Sophia Omary mkazi wa Mbalizi, Stela Mwaluswaswa Mkazi wa Tunduma na Suzana Melele mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya.

Aliwataja  marehemu wengine kuwa ni wanaume waliotambuliwa kwa Bulele Mwaipaja(48) mkazi wa Uyole jijini Mbeya na Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Mbozi Misheni  aliyetambulika kwa jina la Jacob Nyaluke(17).Alisema kati ya majeruhi wa ajali hiyo Wanaume ni 16 na Wanawake 16 hivyo kufanya idadi yake kufikia 32kati yao ambao wamelazwa katika Hospitali za misheni Igogwe na Makandana – Tukuyu.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu katika mfumo wa breki wa gari hilo ambapo dereva aliyefahamika kwa jina la Robert Mwakibibi (37) mkazi wa Uyole  kuacha njia na kasha kupinduka  katika Kijiji cha Kantela Wilayani Rungwe Mkoa wa mbeya.
Aliongeza kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 11:45 asubuhi huko katika kijiji cha Kantela-Ntokela, kata ya Ntokela, tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu ambapo Dereva alikimbia mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Mwisho.1 comment:

Abdulrazak Hatibu said...

Gari aina gani, namba za usajili. Jina la dereva. Gari ilitokea wapi na ilikuwa inaelekea wapi. Habari ikamilike mwanahabari.