Hii ndilo shamba darasa la chuo hicho
Wanachuo 48
wa Chuo cha Kilimo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi
Jijini Mbeya wanakabiliwa na ukosefu wa chakula baada ya uongozi wa Chuo hicho
kuwatelekeza na wao kutokomea kusikojulikana.
Hayo
yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Ilemi Mheshiwa Furaha Mwandalima baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa wanachuo hao na kufika Chuoni hapo na kujionea
hali halisi.
Mwandalima
alichukua hatua za haraka za kumtafuta Mstahiki Meya ambaye alimshauri kutoa
taarifa kwa Mkuu wa Wilila ya Mbeya ili kupata mustakabali wa suala hilo.
Hata hivyo
lilitolewa agizo la kuorodhesha majina ya wanafunzi na mahali wanakotoka ili
kuwarudisha makwao na Chuo kifungwe kutokana na Chuo hicho kutosajiliwa rasmi
na kwamba kilikuwa kinaendeshwa kijanja na wanachuo hao wamelipa malipo ya awli
zaidi ya shilingi laki tano.
Zaidi ya
wanafunzi 40 wanatokea Mkoa wa Kagera na wawili wakitokea mkoani Mara ambapo
wawili wanatokea wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya hali mmoja akitokea Mkoa wa Dar
es Salaam.
Mmoja wa
wanachuo aliyejitambulisha kwa jina la Jenitha Carist alisema waliletewa
taarifa na wakuu wa shule walizokuwa wakisoma baada ya kumaliza kidato cha nne
mwaka uliopita kuwa wamechaguliwa na serikali kusomea Kilimo Mkoani Mbeya
lakini walipofika walishangazwa na hali waliyoikuta na kwamba walipofuatila
kwenye mtandao walibaini chuo kutosajiliwa katika Baraza la Vyuo.
Walipoutafuta
uongozi wa Chuo hicho ulianza kupiga chenga ndipo walikwenda kutoa taarifa
Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo uongozi wa Wilaya umeanza hatua za
kumtafuta mmiliki ili aweze kutoa majawabu.
Hali ilikuwa
tete siku ya Jumamosi ambapo baadhi ya wanachuo walizirai kwa njaa na kulazimu
Diwani Furaha Mwandalima kufanya changizo la dharula na kufanikiwa kukusanya
debe nne za mahindi na maharage debe moja na kuandaa chakula cha dharula
nakuwaandalia mlo wa mchana.
Baadhi ya
majirani walishindwa kujizuia kwa kuangua kilio kutokana na hali mbaya kwa
baadhi ya wanachuo ambapo baadhi walilazimika kuandaa uji ili kutoa msaada wa
haraka.
Kwa upande
wake Diwani Mwandalima amemshukuru Mstahiki Meya Athanas Kapunga na Mkurugenzi
kwa kuhudi zao ili kuwafanya wanachuo hao wafarijike hasa kutokana na wengi wao
kutokuwa na na ndugu na wanatoka mikoa ya mbali.
Mwandalima
ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya kutoa mchango wa hali na mali ili kuokoa maisha
ya wanachuo hao pia amewashukuru wakazi wa Ilemi kwa kuchangia chakula na
mahitaji mengine kwa wanachuo hao.
JE MNAOHUSIKA KUSAJIRI VYUO HIVI MPO? AU MKEKAA TU MAOFISINI KUPIGA SOGA KUSUBIRI MSHAHARA TU MAANA MBEYA KILA KUKICHA VYUO VINAZINDULIWA HEBU WAONEENI HURUMA WAZAZI WANAVYOTABIKA KUITAFUTA ADA KWA AJILI YA WATOTO WAO NA MWISHO WANAAMBIWA CHUO HAKIJASAJIRIWA MWEEE
TAOA MAONI YAKO JUU YA UTAPELI HUU WA VYUO AMBAVYO HAVIJASAJIRIWA
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Huu wote ni ubinafsi na uroho wa pesa na majivuno ya kwamba naweza kumbe hakuna kitu. Ni uwizi kabisa. Mbeya kila kitu ni kibaya tu, hakuna mambo mazuri sana yanayofurahisha kila msiku matukio ya aibu tu. Tubadilike kama wenzetu wa Mwanza na Kilimanjaro
Post a Comment