Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, November 10, 2014

MKUU WA WILAYA YA MBEYA AONGOZA CHAKULA CHA HISANI KUCHANGIA UJENZI WA NJIA ZA KUPITISHIA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA.

MKUU wa wilaya ya Mbeya  Dk. Norman Sigallah King, juzi usiku aliwaongoza wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye  chakula cha hisani ya kuchangia ujenzi wa njia za kupitishia wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Oleais Senga, Akimkaribisha mgeni rasmi

Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo



Subilaga Mwambeta Mkurugenzi AJ Technology moja ya wachangiaji wakubwa wa marafiki wa hospitali ya mkoa Mbeya

Lyimo M.L Meneja Beaco Resort 

Eliah Susuwe   Meneja masoko  AJ Technology

Mganga Mfawidhi wa Hosipitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Grolia Mbwile

Amani Jarafu Simbeye  afisa habari New Focus College Soweto

 Rogers Mwamengo na mkewe Anna Rogers, 








MKUU wa wilaya ya Mbeya  Dk. Norman Sigallah King, juzi usiku aliwaongoza wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye  chakula cha hisani ya kuchangia ujenzi wa njia za kupitishia wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.


Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Beaco iliyopo Forest jijini Mbeya ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya Shilingi Milioni 150 ili kukamilisha ujenzi wa Njia za kupitishia wagonjwa.


Akizungumza na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya, Dk. Norman Sigallah, aliwapongeza Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya sambamba na waanzilishi wa wazo la kujenga njia hizo katika Hospilai hiyo.


Alisema siku zote afya zinapaswa kupewa kipaumbele ili shughuli zingine zziweze kufanikiwa vizuri ambapo pia alitoa wito kwa Wananchi wengine kujitokeza kutoa michango yao ili kukamilisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za waanzilishi wa wazo hilo.


Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Oleais Senga, alisema wazo la awali lilikuwa ni kukarabati paa la Wadi ya akina mama lililokuwa likivuja ambapo baada ya kuchangishana wakaona wasishie hapo bali wajenge na njia za kupitishia wagonjwa.


Alisema mara ya kwanza walichangishana na kupata shilingi Milion 7 ambazo walitoa shilingi milioni moja na kupeleka kukarabati Paa na fedha zingine zilisaidia kuandaa harambee ambayo ilifanyika Mwezi Machi mwaka huu na kupata shilingi Milioni 81ikiwa ni Ahadi na fedha taslimu.

Alisema tangu hapo hatua mbali mbali zilianza kwa kuwapata wasanifu wa kuchora ramani pamoja na Mkandarasi ambapo kazi ilianza bilakujali kiasi cha fedha kilichopatikana.


Alisema hadi sasa Njia ambazo zilipaswa kujengwa zinaurefu wa Mita 405 kati yake Mita 165 zimejengwa kwa kiwango cha sakafu na kuezekwa na mita 104 zikiwa zimesakafiwa bila kuezekwa hivyo kubakiwa na mita 146 ambazo hazijaguswa kabisa.


Alisema hadi sasa kinatafutwa kiasi cha Shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa mita 146, kuezeka mita 104 na kujenza mitaro kwa ajili ya kupitishia maji ya mvua.



Alisema ujenzi huo unafanywa na Mkandarasi wa kampuni ya Inter Frempa Co.Ltd yenye makao makuu jijini Mbeya pamoja na Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST) waliojitolea kuchora ramani ya ujenzi huo bure bila malipo yoyote.


Alisema kujitolea kwa watu hao kumepunguza baadhi ya gharama na kurahisisha ujenzi na kutoa wito kwa wadau kujitoa kwa hali na mali ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati kupitia Mpesa 0762 321829 yenye jina la Marafiki Mkoa au akaunti namba 0150067027600 CRDB jina Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.


Hata hivyo katika Chakula cha Hisani jumla ya shilingi Milioni 26,036,000 zilipatikana zikiwemo fedha taslimu shilingi Milioni 4,646,000 na Ahadi shilingi Milioni 21,390,000/=.


Mwisho.

Na Mbeya yetu



No comments: