Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, November 11, 2014

MGOGORO WA KANISA LA MORAVIA JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAIBUKA UPYA OFISI ZA MAKAO MAKUU JIMBO ZAFUNGWA KWA MINYORORO


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya akiongea na waandishi wa habari nyumbani kwake jimboni hapo akisema sielewi naona tu wakitoa vyombo vyangu nje na kuvuja mabada yangu ya mifugo


Aliyeyeongoza zoezi hilo  Frank Phili Mtunza hazina wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Bethelehem ulioko Mama John Jijini amesema sis tunachotaka Sinodi iitishwe tumechoka na malumbano ya kila kukicha

Mchungaji wa kanisa la moraviani ushirika wa jakaranda akiongea na waandishi wa habari


Baadhi ya Wachungaji na Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Oktoba 10 majira ya saa 11 jioni walifunga ofisi zote za Makao makuu ya Kanisa hilo zilizopo Jacaranda Jijini Mbeya na kumzuia aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya kuhama kwenye eneo hilo kwenda nyumba nyingine eneo la Saba saba.

Aliyeyeongoza zoezi hilo ni pamoja na Frank Phili Mtunza hazina wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Bethelehem ulioko Mama John Jijini Mbeya akiwa na Mchungaji Mwilgumo pamoja na Mchungaji Mwakyoma.

Ofisi zilzofungwa kwa kutumia minyoro na mbao ni pamoja na ofisi ya Askofu Alinikisa Cheyo,Ofisi ya Katbu Mkuu,Ofisi ya Mtunza Hazina Mkuu na lango kuu la kuingilia makao makuu ya Kanisa hilo.

Hatua hii ya kufunga ofisi za Kanisa ni la pili kwa mwaka huu awali ilikuwa mwezi Julai mwaka huu ambapo waumini hao walifunga hivyo hivyo kabla ya Serikali kuingilia kati na kufanya suluhishi kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya na kuweka makubaliano.

Hata hivyo Phili alidai maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama hayakutekelezwa ikiwa ni pamoja na kumrudisha kazini Mchungaji Nosigwe Buya na kuacha kumhamisha kituo cha kazi.

Aidha waumini hao walichukua hatua ya kuzuia kuhamishwa kwa Mchungaji Buya ambapo alikuwa amefunga mizigo yake huku mkewe akishindwa kupika na kuwahudumia watoto kwa siku nzima na banda la mifugo limeezuliwa na mtu aliyetumwa kutoka ofisi kuu.

Pamoja na juhudi za Kanisa kujaribu kumhamisha Mchungaji Nosigwe Buya ziligonga ukuta baada ya ya waumini hao wasiozidi ishirini kumuondoa kijana aliyekuwa akiondoa mabati na mabanzi ya banda la mifugo kuondoka mara moja na kumtaka mke wa Mchungaji Buya Edda Kabuka kuendelea na shughuli zake.

Kwa upande wake Mchungaji Buya alisema kuwa hapingi kuondoka katika nyumba hiyo na kukataa kwenda kituo kingine cha kazi lakini ameshangazwa na kwenda kinyume na makubaliano ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya lakini kukiukwa maazimio ya yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu.

Pia alidai mgogoro huu umeligawanya Kanisa na kwamba hivi sasa mahubiri yanayofanyika kanisani yamekuwa ya kutpiana maneno kwa pande mbili zinazopingana na kufanya waumini kushindwa kupata ufumbuzi wa kudumu na kudai kuwa suluhu pekee iwe ni kuitisha mkutano mkuu wa Kanisa(Sinodi).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema amesikitishwa na pande hizo zinazopingana na kwamba ni kwa nini mgogoro huo haupati ufumbuzi licha ya Kamati ya ulinzi na usalama kusuluhisha na kwamba Jeshi la Polisi litamkamata yeyote atakayevunja amani kwani kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa Raia na mali zake.

Na Mbeya yetu


2 comments:

Akwino Msombe said...

MBONA HATARI HII

Anonymous said...

Very embarrassment kwa kanisa. Nini kinachowafanya msikae pamoja na kumaliza ugomvi wenu. Aibu sana kwa kanisa kuwa na malumbano. Tutasaidianje malumbano ya kisiasa?