.Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela
akikagua vifaa vya maabara pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Tukuyu,
Tiberi Sambala
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imejipanga kuhakikisha inatekeleza agizo la
Rais la ujenzi wa Maabara katika Shule za Sekondari ifikapo Novemba 15 Mwaka
huu linakuwa limekamilika.
Hayo
yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela, alipokuwa
akipokea msaada wa mifuko ya Saruji kutoka kampuni ya uzalishaji na uchimbaji
wa gesi Mkaa ya TOL Gases limited na Mradi wa huduma ya umeme vijijini (REA)
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara wilayani hapo.
Meela
alisema msaada huo umefika katika kipindi muafaka ambapo Halmashauri inajipanga
kuhakikisha agizo la ais la kujenga maabaraNchi nzima linakamilika hadi ifikapo
Novemba 15 mwaka huu ambapo alisema tayari ujenzi huo umefikia zaidi ya
asilimia 80.
Akiyashukuru
makampuni hayo Meela alisema ni makampuni yanayoshughulika na masomo ya sayansi
hivyo michango yao ni kuongeza chachu ya upatikanaji wa wataalamu katika
shughuli zao wanazozifanya ili waweze kuongeza wengine wengi kupitia shule za
Kata.
Alisema
katika kutekeleza agizo hilo, Wakuu wa Idara wote wamepelekwa kwenye maeneo ya
ujenzi ili kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha malengo yanatimia kama
ilivyopangwa ambapo Halmashauri ina sule 43 ambazo zinatakiwa kujengwa maabara.
Aliongeza
kuwa baadhi ya watu wanafikiri agizo la Raisi ni ujenzi wa majengo ya maabara
pekee lakini Halmashauri yake imeshakamilisha ujenzi wa majengo na kilichobaki
ni miundombinu inayopaswa kuwekwa kwenye maabara ili ianze kufanya kazi jambo
ambalo alisema litakuwa limekamilisha kabla ya muda.
Alisema
hivi sasa wanajipanga kuhakikisha wanajaza vifaa vya maabara ikiwa ni pamoja na
kununua mitungi ya Gesi upatikanaji wa umeme kwa shule zilizopitiwa na Grid ya
Taifa huku wakiomba msaada Wizarani wa kupata Umeme wa Jua kwa shule zilizoko
vijijini ili maabara ziweze kufanya kazi kisasa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya State Grid Company ltd inayohusika na
mradi wa umeme wa Rea, Andrew Mwaipaja, alisema wameguswa kuchangia kutokana na
kinachohimizwa kunahusiana na kazi yao ya kuitaji mafundi na wataalamu wa
sayansi ambao watapatikana baada ya kuwa na maabara nzuri.
Alisema
Kampuni yake imeguswa na kuamua kuchangia mifuko 100 ya Saruji pamoja na
Seiling Bod 80 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni tatu ambavyo
vilikabidiwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe.
Naye
Mkurugenzi wa Fedha wa TOL Gases ltd, Evarist Tilafu, alisema wamuamua
kuchangia mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya shilingi Milioni 1.7 kama
sehemu ya uwajibikaji kwa jamii ambayo ipo jirani na eneo wanalifanyia kazi.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment