Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, November 18, 2014

HALI YA MGOGORO WA KANISA LA MORAVIAN BADO MBICHI.

Askofu wa Jimbo wa Jimbo la Kusuni Magharibi, Alinikisa Cheyo,


SINTOFAHAMU ya mwisho wa mgogoro unaondelea ndani ya Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi imeendelea kuwakumba waumini wa kanisa hilo licha ya Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa kuagiza litafutiwe ufumbuzi wa haraka.

Hali hiyo imeonekana kushindwa kupata muafaka baada ya Mkutano wa Halmashauri kuu ya Jimbo kuvurugika na hatimaye kuusogeza mbele baada ya kutokea kutoelewana.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake , Askofu wa Jimbo wa Jimbo la Kusuni Magharibi, Alinikisa Cheyo, wakati akitoa taarifa ya Halmashauri kuu ya Kanisa kuhusu mgogoro katika mkutano uliofanyika Novemba 15 mwaka huu Vwawa mkoani Mbeya alisema baada ya mkutano kuvurugika ukasogezwa mbele hadi Disemba 16, mwaka huu utakapofanyika tena.

Askofu Cheyo alisema mkutano huo ulifanyika baada ya kutoa tamko novemba 11, mwaka huu la kuitisha Halmashauri kuu kufuatia mgogoro unaoendelea ndani ya kanisa hilo na kusababisha baadhi ya waumini kufunga ofisi kwa minyororo na kusababisha Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuingilia kati.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya kanisa aliwaagiza kamati tendaji kuwaatarifu wajumbe wote wa halmashauri kuu ya Jimbo kuhudhuria Mkutano wa Novemba 15 mwaka huu.

Alisema pia aliagiza katika mkutano huo barua iliyoandikwa na Mchungaji Buyaya julai 28, mwaka huu aliyoiandika ya kuomba msamaha ili halmashauri kuu irejee kwa upya kuangalia maudhui ya barua hiyo na kutafuta uwezekano wa kumaliza mgogoro huo kwa nia ya kusameheana.

Alisema kamati tendaji ilitekeleza kile alichokiagiza isipokuwa barua ya Mchungaji Buya kwa madai kuwa hawakuona sababu ya kuleta barua hiyo kwa sababu Askofu alitoa tamko la kuitisha mkutano huo kinyume cha Katiba ya Kanisa sehemu ya V ibara ya 34,b,vi ya mwaka 2012.

Alisema kutokana na majibu hayo ndipo hali ya kutoelewana ndani ya mkutano iliapoanza kuibuka na kuhatarisha hali ya usalama hali iliyomlazimu Askofu kujitetea kuwa alitoa tamko kwa mujibu wa Katiba ya Moravian duniani (Church order of the unitas fratrum chapter XIII,A,2,C of 2009) ambayo inasema Askofu ana mamlaka ya kutamka kwa niaba ya kanisa na maoni ya askofu yanapaswa kuzingatiwa na kanisa.

Alisema mgogoro ndani ya mkutano ulizidi kupamba moto baada ya Kamati kusisitiza msimamo wao huku baadhi ya wajumbe wakigawanyika kuhusu kumrudisha Makamu Mwenyekiti madarakani na wengine wakipinga wakidai hata akirudishwa atafanya kazi katika mazingira magumu.

Aliongeza kuwa baada ya mvutano mkali ikaamliwa Disemba 16, mwaka huu maamuzi rasmi kuhusu mgogoro na mustakabari wa kanisa vitatolewa na Hlmashauri kuu.

Askofu alisema kulingana na kikao hicho kuanzia sasa msemaji wa kila jambo linaloendelea ndani ya kanisa atakuwa Makamu Mwenyekiti Mchungaji Zakaria Sichone hadi muafaka utakapopatikana na amani kurejea ndani ya Kanisa.

Alisema pamoja na kukubaliana maamuzi kutolewa Disemba 16, mwaka huu, pia ameona aitishe mkutano na kamati ya ushauri ya Jimbo ili kuwaeleza hali ya Kanisa ilivyo sasa pamoja na kukutana na kamati teule ya usuluhishi wa migogoro ya jumuiya ya kikristo Tanzania inayoongozwa na Askofu mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa akisaidiwa na Jaji mstaafu Agustino Ramadhani ili wafanye haraka kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro huo ili kuzuia uvunjifu wa amani katika kanisa.

Mwisho. 

Na Mbeya yetu


2 comments:

Anonymous said...

Kuna watu wamedhamiria kabisa kulitesa kanisa. Hivi ni kwanini mtu anayejiita mchungaji aendelee kung'ang'ania cheo wakati ametakiwa atoke? Kuna maslahi gani jamani?

Anonymous said...

Kuna watu wamedhamiria kabisa kulitesa kanisa. Hivi ni kwanini mtu anayejiita mchungaji aendelee kung'ang'ania cheo wakati ametakiwa atoke? Kuna maslahi gani jamani?