Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 24, 2014

MKUU WA MKOA WA MBEYA APOKEA TAARIFA YA SAFARI YA WAANDISHI WALIOFANYA ZIARA NCHINI MALAWI.

 Mwenyekiti wa Msafara, Ulimboka mwakilili akimkabidhi mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro taarifa ya safari ya Malawi
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akipokea baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya Waandishi wa habari waliofanya ziara nchini Malawi
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa pongezi kwa waandishi waliofanya ziara nchini Malawi mara baada ya kupokea taarifa yao
Mratibu wa Ziara ya waandishi nchini Malawi, Venance Matinya, akisoma taarifa ya safari kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro 


Baadhi ya Waandishi wa Habari sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa makini taarifa ya safari inayosomwa na mratibu wa ziara Venance Matinya. Mmoja kati ya Waandishi waliofanya ziara nchini Malawi, Christopher Nyenyembe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya msafara mzima kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
 Hiki ni kikosi kizima cha Waandishi waliosafiri kwenda na kurudi nchini Malawi kwenye ziara ya kimafunzo iliyofanyika hivi karibuni.
 Viashiria vya kutambulisha miji ya malawi kama inavyoonekana

 Waandishi wakiwa nchini malawi walifanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utalii na utamaduni wa Malawi kwa niaba ya Rais
 Waziri wa Habari Utamaduni na Utalii wa Malawi Kondwan Nankhumwa, akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya (hawaonekani pichani)

 picha ya pamoja na Waziri
 Waandishi wa habari kutoka mbeya wakiwa wameungana na Waandishi wa habari wa Mzuzu nchini Malawi katika picha ya pamoja na Meya wa Jiji la Mzuzu Wiliam Mkandawile.

 Vyakula vya asili pia vililiwa tukiwa njiani kuelekea jijini Lilongwe

 Mnara wa kumbukumbu ya Raisi wa kwanza wa Nchi ya Malawi
 Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere akipokea Picha ya Mbeya City ili itangazwe kimataifa 
Balozi Tsere akifurahia jambo na waandishi
 Mazungumzo na Balozi Tsere
                                                                                Baadhi wakipongezana kwa kufika salama nchini Malawi.MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewapongeza Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kwa kuiwakilisha vizuri nchi katika ziara walioifanya nchini Malawi hivi karibuni.

Kandoro alitoa pongezi hizo alipokuwa akipokea taarifa ya Safari hiyo, katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake ikijumuisha baadhi ya waandishi waliokuwa wamesafiri nchini Malawi.

“Nawapongeza sana mmeiwakilisha Nchi vizuri kwa kupokelewa na kurudi salama pia kutangaza vivutio vyetu kwa majirani hususani uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe” alisema Mkuu wa Mkoa.

Alisema Serikali itaerndelea kukuza ushirikiano na Nchi jirani hususani katika biashara kwa kubadilishana bidhaa mbali mbali za mazao pamoja na kuwaomba kuutumia uwanja wa Ndege wa Songwe katika safari zao.

Aidha alipongeza suala la mipango miji na kwamba Serikali inapaswa kuiga kwa kutenga maeneo na kuhamasisha upandaji miti.

Na hii ni sehemu tu ya taarifa iliyowasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa.

“Waandishi wa habari wapatao 12 wa Mkoa wa Mbeya walifanya ziara nchini Malawi kuanzia Septemba 14 hadi 19, 2014 na kufanikiwa kutembelea miji mbali mbali ikiwa ni pamoja na Jiji la Mzuzu na Lilongwe.

Madhumuni ya safari hiyo ilikuwa ni kufanya ziara ya mafunzo(study tour), kutembelea sehemu za vivutio na maeneo ya kihostoria yaliyoko nchini Malawi na kutangaza vivutio vinavyopatika nchini Tanzania hususani Mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Pia kuimarisha uhusiano wa Waandishi wenyewe kwa wenyewe, Nchi na nchi, kushirikiana kutangaza vivutio vya utalii, kuandika habari kwa pamoja zinazohusu usalama wa mipakani, mazingira, uchumi na Ukimwi.

Waandishi walioweza kumudu safari hiyo kutokana na gharama za kuchangia ni Venance Matinya(Jamboleo), Ulimboka Mwakilili(Mbeya press), Brandy Nelson(Mwananchi),Christopher Nyenyembe(Tanzania Daima),Felix Mwakyembe(Raia mwema), Joseph Mwaisango(Mbeya yetu blog),Rose Chapewa(Chanel ten), Rashid Mkwinda(Majira), Fred njeje(Tone mult media), Ezekiel kamanga(Bomba fm), Henry Mazunda(Baraka fm) na Claudio Rusimbi mlezi wa Mbeya press club.”

               Na    Mbeya yetuNo comments: