Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, October 5, 2014

MKUTANO WA WAHITIMU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) WANAOISHI NYANDA ZA JUU KUSINI WALIO SOMA CBE KUANZIA MWAKA 1965-2014 IKIWA NI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO JIJINI MBEYA .

Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile ambaye ndiye Mgeni Rasmi katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanaoishi nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka 1965-2014 na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye alisoma katika chuo hicho mwaka 1967 na ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi katika chuo hiki na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za juu kusini akitoa hotuba yake ambapo, alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja pia aliongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu hata Viongozi baadhi yao Tanzania wamesoma katika Chuo hicho mfano Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Stagomena Tax Katibu Mtendaji SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dkt. Ramadhani Dau Mkurugenzi Mtendaji NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA kanda za nyanda za juu Kusini , Alimalizia kwa Kuzindua umoja huo wa wanafunzi na kusema CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi . Mwisho alizindua Rasmi Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu kusini mkutano uliofanyika Tarehe 4.10.2014
 Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo
Meza kuu
 Muongozaji wa Mkutano MC Bwana Ben akiwa anatoa Muongozo wakati wa Mkutano huo 
 Mkuu  wa Chuo Cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya Ndugu Deonise Lwanga akitoa utambulisho pamoja na Kumkaribisha Mkuu wa Vyuo vyote vya CBE Tanzania.
 Mkuu wa Vyuo vyote vya Elimu ya Biashara (CBE ) Profesa Emmanuel Mjema akitoa nasaha zake na kueleza malengo makuu ya Mkutano huo, alieleza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE kuwa ni Mabalozi wazuri ambao ndio wanaweza kukitangaza vyema chuo hicho kwa kuwa wao ndio wanajua vyema chuo hicho, aliongeza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE wanasaidia chuo kwa kutoa mrejesho wa chuo hicho,pia inasadia katika Elimu, na aliongeza kuwa Alumni ni muhimu katika maswala ya kuandaa Semina, Makongamano na mambo kama hayo, Mwisho Alimshukuru Mgeni Rasmi kwa kukubali mwaliko na kujumuika katika Mkutano huo pamoja na wanachuo wote waliowahi kusoma katika chuo cha CBE
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Mipango, Fredha na Utawala Dkt. Peter Msami akitoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya chuo cha CBE
 Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo cha CBE Bwana John Mwangobola akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za juu Kusini ambao umezinduliwa Rasmi Tarehe 04.10.2014 Bwana Boyd Faustin Mwakyusa akitoa neno la Shukurani Baada ya uteuzi huo
Msimamizi wa Taaluma kutoka Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya Bwana Kayombo akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
 Viongozi wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu Kusini wakiwa pamoja na Mlezi wao Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile wa nne Kutoka Kushoto Mara baada ya Uchaguzi huo
 Washiriki wakiwa wanafuatilia Mkutano kwa umakini
Picha ya Pamoja

Na Mbeya yetu


3 comments:

AMINA said...

Waje hao CBE watuboreshee biashara zetu mtaani.

Anonymous said...

Mheshimiwa Lwanga, tumeziona juhudi zako. Hongera sana MUNGU akuwezeshe ili Kampasi ya Mbeya iwe mfano wa kuigwa na kampasi zote, na vyuo vingine pia. Tunatambua juhudi na uwezo wako toka ukiwa SBC Tanzania (PEPSI), hivyo tuna uhakika si muda mrefu utaanza kutoa shahada.

Anonymous said...

It's a good start by association with the past graduant. The new team should focus on competitive advantage by being creative and innovative