Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 3, 2014

CHADEMA MBEYA WAMPINGA RPC MSANGI, YEYE MWENYEWE ADAI ANAGOMBANISHWA NAO.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo alikataa vikali kwamba hakuwahi kuitoa na hawezi kutoa kauli kama hiyo kutokana na wadhfa alionao.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu) wa pili kulia akiongea na waandishi wa habari 

Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya wakiwa katika kikao hicho



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya mjini, kimpe siku tatu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi kukanusha kauli yake kuhusu kuwashughulikia Chadema wakifanya maandamano.

Viongozi hao wa Chadema wakiongozwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu) wametoa kauli hiyo  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peak kufuatia baadhi ya magazeti kumnukuu kuwa atakaye andamana atafanyiwa kitu kibaya ambacho hataweza kusahau maishani mwake.

Akitoa ufafanuzi juu ya Mkutano huo, Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbeya mjini, Christopher Mwamsiku, alisema Chama kimelazimika kuitisha mkutano na vyombo vya habari ili kukemea kauli aliyoitoa Kamanda wa Polisi na kunukuliwa na baadhi ya magazeti.

Alisema Kauli aliyoitoa Kamanda Msangi dhidi ya Chadema  kwamba atakayeandamana atafanyiwa kitu kibaya ambacho hawatakuja kukisahau katika maisha yao haipaswi kufumbiwa mdomo.


Awali akitoa Tamko kwa niaba ya Chama, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema kama chama kinatoa siku tatu Kamanda Msangi awe ameomba radhi kwa matamshi yake hayo.

Alisema endapo atashindwa kuomba radhi, Chama kiko tayari kuanza kukabiuliana naye kwa namna yoyote ile kwa maana wanaamini Msangi hana Jeshi, Siraha, Bunduki na mabomu ya kuweza kuwashinda Chadema wakiamua kupambana naye.

Alisema hivi sasa Redbriged ya Chadema imeshafanya sense ya Askari wanaoishi uraiani pamoja na kuzitambua nyumba wanazoishi ili akishindwa kuomba radhi watawalazimisha kurudi kwenye kota za polisi.

Alisema kufanya hivyo ni kuwanusuru endapo viongozi wa Chadema watapatwa na tatizo lolote hawataweza kunusurika kwa kile Chadema itakachoamua kukifanya dhidi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.


Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo alikataa vikali kwamba hakuwahi kuitoa na hawezi kutoa kauli kama hiyo kutokana na wadhfa alionao.

Alisema hayo maneno na yeye pia aliyasoma kwenye gazeti kama Chadema walivyosoma hivyo hatua ya kwanza aliyoichukua ni kuwapigia simu wahusika wa gazeti akiwalalamikia kumlisha maneno ambayo hakuyasema.

Alisema anachokumbuka ni kwamba Mwandishi wa habari hizo amewahi kumuuliza kuhusu kuwepo kwa maandamano ya Chadema kupinga Bunge la Katiba nayeye kumjibu kuwa maandamano yamekatazwa kote nchini hivyo atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kauli hiyo inalengo la kuligombanisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Chadema lakini yeye binafsi naushirikiano wa karibu na viongozi wa Chademana na kuongeza kuwa yeye sio kiongozi wa Mtu mmoja bali kila mwananchi aliyepo Mbeya bila kujali chama anachotoka.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: