Amon Mwamtobe ni Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara ndogondogo minadani akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani |
Baadhi ya viongozi wa umoja huo walioandamana na mwenyekiti huyo |
Hii ni hati ya usajiri wa chama chao |
Moja ya majukumu ya umoja huo kusimamia upakiaji wa mizigo na wafanyabiashara wanaoenda mnadani kama mnavyoona kwenye picha hiyo hapo juu ............................................... |
UMOJA wa wafanyabiashara ndogondogo
minadani Mbeya (UWABINDOMI) wanaziomba taasisi mbali mbali ndani na nje ya Mkoa
wa Mbeya kuwasaidia kuwapa usafiri.
Wafanyabiashara hao wapatao zaidi ya
10,000 kutoka Kanda za Chunya, Mbarali, Mbozi na Sumbawanga wamesema huduma zao
ni kupeleka bidhaa vijijini kwa njia za minada kutokana na baadhi ya maeneo
kutofikiwa na wafanyabiashara wenye maduka.
Wakizungumza na waandishi wa habari hivi
karibuni, baadhi ya viongozi wa Umoja huo walisema umoja wao umesahauliwa
tofauti na vyama vingine ili hali wao wamekusanya kundi kubwa la watu.
Walisema kundi wanaloshughulika nalo ni
kubwa ambalo lingeachwa lingekuwa chanzo cha kukithiri kwa uhalifu katika
majumba ya watu lakini wameweza kuwakusanya na kusafiri nao minadani.
Amon Mwamtobe ni Mwenyekiti wa Umoja huo
anasema tangu kuanzishwa kwa umoja huo hali ya uhalifu imepungua kutokana na
kuwakusanya wafanyabiashara ndogo ndogo kama vile Machinga ambao wamekuwa
wakinyanyaswa mijini.
Alisema watu wengi hawautambui umoja huo
ambao upo kisheria na kusajiliwa kwa namba SA 17148 na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya nchi hivyo wametoa wito kwa Serikali na watu binafsi kuona haja ya
kuwasaidia kwa hali na mali.
Alisema changamoto kubwa inayowakabili
ni ukosefu wa usafiri wa magari ya kupeleka bidhaa minadani kutokana na wingi
wa wafanyabiashara na bidhaa wanazobeba.
Alisema asilimia kubwa ya
wafanyabiashara hao mitaji yao ni midogo hivyo kushindwa kumudu gharama za
kukodi magari kwa ajili ya kwenda vijijini kufanya minada ya biashara zao.
Mwamtobe alisema ni vema kama
Serikali ama taasisi yoyote yenye uwezo wa kuwasaidia magari ya mizigo au
kuwakopesha ili waweze kulipa taratibu wakafanya hivyo ili kuikomboa jamii
iliyoko pembezoni kutokana na kutofikiwa na bidhaa mbali mbali.
Alisema wananchi vijijini wameshazoea
kupata mahitaji yao kutoka minadani kutokana na kutokuwa na maduka pia umbali
uliopo kutoka vijijini hadi kuyafikia maduka yaliyoko mjini ili kununua
mahitaji ya kila siku.
Alisema Umoja wao unauwezo wa kulipa
gharama za gari kidogo kidogo endapo watapa mdhamini atakayeweza
kuwaunganisha na wafanyabiashara wakubwa wanaouza magari.
Kwa atakayeguswa na mahitaji ya umoja
huu anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti kwa namba 0757 354326 kwa ajili ya
msaada wa kupata magari ya kusafirishia bidhaa kupeleka minadani.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment