Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, September 6, 2014

KWA MWENDO HUU AFYA ZETU ZITAKUWA SALAMA? WAHUSIKA WA AFYA MBEYA MPO?

Hapa ni Kiwira-Tukuyu Mkoani Mbeya.. Kamera ya Mbeya yetu ilifanikiwa kuwanasua hawa Jamaa ambao walikuwa wametoka na Utumbo wa Ng'ombe Machinjioni na kuusafirisha Kienyeji kama hivi huku ukiburuzwa Chini ambapo watu, wanyama na matakataka yapo hapo chini, Wakati hup huo haujafunikwa na kitu chochote unapigwa vumbi na wanaousafirisha ndio hao wanavyo onekana hawana hata dalili za kujali Afya na Mwisho wa Siku utombo huo huo unakuja kutumika na Binadamu, kwa matumizi ya Mboga au Supu katika migahawa na watu wanafurahia na huku wasijue hivi ndivyo unavyo safirishwa.
Sasa Mbeya yetu Tunapenda kuuliza swali hasa kwa hawa wahusika wa mambo ya afya je swala hili wanalitambua? Je hakuna vifaa Maalum vya kusafirishia hizi Mboga? kama vipo mbona visitumike?

Na kwa watumiaji wa Mboga hii je Hili swala mnalizungumziaje? karibuni kwa maoni.

Picha na Mbeya yetu Blog

4 comments:

Anonymous said...

Jamani hata kuweka kwenye visafeti manake ukisema kwenye ndoo bado wataona ni ghali, please watu wa afya jamani tumechoka na magonjwa!!!!!

Anonymous said...

Hatari sana

raphael said...

nisheeeda kwakwel

Anonymous said...

Kwa kweli mamlaka ya afya ichukue tahadhari juu ya suala hili. Huku ni kuendekeza uzembe wa kulinda afya za watu na kujali maslahi yako binafsi. Ni hatari