Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 6, 2014

WENGI WANEEMEKA NA BANDA LA TIA NANE NANE MBEYA

 Wanafunzi wakiwa wanapata elimu katika Banda la TIA
 Elimu ikiendelea kutolewa katika Banda la TIA

 Wanafunzi wakiendelea kupata elimu jinsi ya kujiunga na Chuo hicho

************
IJUE TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY
(TIA)

Taasisi ya Uhasibu Tanzania yaani TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) ni Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Fedha iliyopewa jukumu la kutoa mafunzo katika nyanja za Uhasibu, Ununuzi & Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu,Masoko &Uhusiano, Uhasibu wa Fedha za Umma na nyanja nyingine za biashara kwa ngazi ya Cheti cha Awali, Stashahada, Shahada , na Stashahada ya Uzamili

TIA imesajiliwa na  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na inatambuliwa na Bodi za Kitaaluma kama vile Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA)na Bodi ya Wataalam na Wasimamizi wa Vifaa na Ugavi (PSPTB);  hivyo kuwanufaisha wahitimu wa fani husika. 

TIA ina Kampasi tano zikiwa na jumla ya wanafunzi elfu kumi na nne na thelatini (14,030). Kampasi hizi zipo katika mikoa ya Dar es Salaam (ambayo ni Makao Makuu), Mbeya, Singida, Mtwara, na Mwanza, ili kuwafikia wateja wake kwa urahisi.  Katika kutimiza azima hiyo, kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ambao utaanza mwezi septemba 2014 Taasisi imefungua Kampasi katika mkoa wa Kigoma na hivyo kufanya idadi ya Kampasi kuwa sita.

Dira ya Taasisi:
“Taasisi kuwa chaguo la wengi katika kutoa elimu ya juu ya biashara nchini” 
Dhima ya Taasisi:
Kutoa elimu bora, utafiti na ushauri katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Teknolojia ya Mawasiliano na katika Nyanja nyingine za biashara.

MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA:

1.    Nifanyeje ili kujiunga na TIA?
Ukitaka kujiunga na Taasisi ya Uhasibu Tanzania unatembelea tovuti yetu ambayo ni www.tia.ac.tz. Fomu za kujiunga na Taasisi zinapatikana katika tovuti hiyo. Utajaza fomu kisha utalipia sh. 20,000/= (gharama ya fomu) katika tawi lolote la NMB kwenye akaunti namba 2061100017 jina la akaunti ni Chief Executive Officer, Tanzania Institute of Accountancy. Fomu iliyojazwa itaambatanishwa na “pay in slip” ya benki, vivuli vya vyeti pamoja na picha moja na kurudishwa katika kampasi yoyote iliyo karibu nawe kama anuani za Kampasi zetu zilizopo chini ya tangazo hili zinavyoonyesha.

2.    Nitafahamuje kama nimepata nafasi TIA?
Taasisi inapenda kuwatoa wasiwasi wa kukosa nafasi wale wote wanaoomba kujiunga na TIA katika kozi mbalimbali. Hii ni kutokana na Taasisi kuwa na Kampasi za kutosha zilizopo katika mikoa sita. Kwa kawaida majina ya wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Taasisi huwekwa kwenye tovuti yetu www.tia.ac.tz lakini pia tunatoa taarifa kupitia magazeti mbalimbali. Orodha hii ya majina ya waliochaguliwa, hutolewa kwa awamu tofauti tofauti kadiri maombi yanavyoendelea kupokelewa. Kwa utaratibu wetu wa sasa, unaporudisha fomu, kama unakidhi vigezo unapata barua ya udahili (admission letter) hapo hapo.

3.    Nina uhakika gani kama nitapangwa kwenye Kampasi niliyoichagua?
Kila mwanafunzi hupangwa kusoma kwenye kampasi kulingana na uchaguzi aliofanya wakati anajaza fomu ya kujiunga na Taasisi. Ikitokea umepangwa Kampasi tofauti, tafadhali toa taarifa mapema ili ufanyiwe uhamisho.

4.    Mimi ni mwajiriwa na siwezi kupata ruhusa ya kusoma, je, TIA itanisaidiaje?
Mafunzo yetu huendeshwa kwa mfumo wa kutwa na jioni hivyo kumwezesha hata mwajiriwa kupata fursa ya kujiendeleza kimasomo.


5.    Kwanini nichague kusoma TIA?
TIA inatoa elimu iliyo bora, ina wahadhiri na wafanyakazi wenye sifa na wanaojituma huku mazingira mazuri ya kusomea na nyenzo nyingine muhimu za kufundishia zilizo katika Kampasi zake zote kuwapatia wanafunzi elimu bora na si bora elimu. Wahitimu wetu wanakubalika katika soko la ajira na hivyo kuajiriwa kwenye sekta za umma na binafsi. Sanjari na hilo, Ada zetu ni nafuu sana ukilinganisha na ubora wa elimu tunayoitoa na pia ukilinganisha na vyuo vingine vilivyo katika kiwango chetu.

6.    Nifanyeje ili nichaguliwe kusoma TIA katika ngazi ya Shahada ya Kwanza?
Ukitaka uchaguliwe kusoma TIA, ukiingia kwenye mtandao wa TCU ambao ni www.tcu.go.tz (kwa waliomaliza kidato cha sita) au mtandao wa NACTE ambao ni www.nacte.go.tz (kwa wenye Diploma), hakikisha TIA inakuwa chaguo lako la kwanza. Ikitokea katika orodha ya majina umepangwa kwenye chuo kingine badala ya TIA, tafadhali fika katika ofisi zetu pindi orodha inapotolewa ili ufanyiwe utaratibu wa kuhamishwa.

Kwa Mawasiliano na taarifa zaidi kuhusu Tanzania Institute of Accountancy, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

MAKAO MAKUU:
Afisa Mtendaji Mkuu,
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),
Kurasini, Makutano ya Barabara ya Kilwa/Nelson Mandela,
S.L.P. 9522, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2851035/6; 0754376371, 0714914805
Nukushi: +255 736 502630
Barua pepe: tia@tia.ac.tz
Tovuti: www.tia.ac.tz


KAMPASI YA MBEYA:
Meneja wa Kampasi,
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) - Mbeya,
Mwanjelwa, Makutano ya Barabara ya Uwanja wa Ndege wa zamani/Zambia,
S.L.P. 825, Mbeya
Simu: 025 2502276; 0756273552, 0753877652
Nukushi: 025 2503057
Barua pepe: tiambeya@tia.ac.tz

KAMPASI YA SINGIDA:
Meneja wa Kampasi,
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) - Singida
Barabara ya Sepuka,
S.L.P. 388,Singida
Simu: +255 26 2502125; 0754486044, 0713418283
Nukushi: +255 26 2502844,

KAMPASI YA MTWARA:
Meneja wa Kampasi,
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) - Mtwara
Uwanja wa Sabasaba,
S.L.P. 169, Mtwara
Simu: +255 23 2333948; 0755397449, 0767568807
Nukushi: +255 23 2333948,

KAMPASI YA MWANZA:
Meneja wa Kampasi,
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) - Mwanza
Barabara ya Musoma, eneo la Nyakato, Jirani na kituo cha mabasi cha Buzuruga,
S.L.P. 5247, Mwanza
Simu: +255 28 2570475; 0754443930, 0786801223
Nukushi: +255 28 2570475,

KAMPASI YA KIGOMA:
Meneja wa Kampasi.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) - Kigoma
Barabara ya Lumumba Mjini Kigoma Ujiji, Jengo la WFP la zamani (linatazamana na jengo la Uhamiaji Mkoa wa Kigoma),
Simu: +255 713 046 466, 0715260499
Barua pepe: tia@tia.ac.tzNo comments: