Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 25, 2014

WAANDISHI WA HABARI MBEYA WAISHUKIA TMF

Afisa Ruzuku kutoka TMF akifungua semina kwa waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Washiriki wa semina wakiwemo maafisa wa TMF na Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa makini

BAADHI ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wametoa duku duku lao kwa Mfuko wa vyombo vya habari nchini(TMF) kuhusu utaratibu wa kupata ruzuku kwa ajili ya kufanya kazi za uchunguzi.
Malalamiko hayo yalitolewa jana mbele ya viongozi wa TMF katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa GR Hotel iliyopo Soweto jijini Mbeya ambapo waandishi wa Habari walipata fursa ya kutoa ya moyoni.
Awali Afisa Ruzuku wa TMF, Japhet Sanga, katika utangulizi wake aliuliza idadi ya waandishi waliowahi kunufaika na Mfuko huo kwa Mkoa mzima tangu uanzishwe ambapo waandishi sita waliweza kujitokeza.
Kutokana na idadi hizo Afisa huyo alizidi kuhoji ni kwanini idadi iwe ndogo kiasi hicho ukilinganisha na utitili wa Waandishi wa Habari uliopo Mkoa wa Mbeya.
Wakichangia hoja baadhi ya waandishi walisema wanahisi kuwepo kwa hali ya upendeleo kwa baadhi ya waandishi kujirudia kupata ruzuku aidha kwa kuangalia majina ama kupata chochote kutoka kwa mwandishi(ten percent).
Hata hivyo changamoto nyingi zilizozungumzwa na Wanahabari, Afisa Ruzuku alisema zimechukuliwa na kufanyiwa kazi kisha kuendelea na ufafanuzi juu ya namna ya kuomba ruzuku kwa kufuata vigezo na masharti.
Na Mbeya yetu Blog

No comments: