Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, August 2, 2014

TANGAZO ! TANGAZO ! TANGAZO! MPYA : EZEE MONEY MKOMBOZI WA MFANYABIASHARA NCHINI. Moja ya mashine za Ezey money katika muonekano wake baada ya kuwashwa.

Kampuni ya New position co.ltd yenye makao makuu jijini Mbeya ikishirikiana na Kampuni ya kimataifa ya Ezee Money limited imeleta mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa  kumkomboa mfanyabiashara.

Mashine hiyo inayojulikana kwa jina la EzeeMoney ni mashine iliyotengenezwa  nchini Malaysia kwa ajili ya kurahisisha shughuli mbali mbali za kifedha na kibiashara.

Meneja wa Kampuni ya New position ambao pia ni Mawakala wa ajira Mkoa wa Mbeya, Juma Bura, akizungumzia ujio wa mashine hizo amesema ni msaada mkubwa kwa jamii kutokana na kurahisisha vitu vingi.

Amevitaja baadhi ya vitu vinavyotumiwa na mashine hizo kuwa ni pamoja na kumrahishia mwanamchi badala ya kutembea na fedha taslimu katika mahitaji mbali mbali anaweza kuwa na kadi ya Ezee Money na akamaliza huduma zake zote.

Wafanyabiashara wenye maduka ya makubwa ya jumla na rejareja, Supermarket, Pharmacy, Hotel na Baa wanaouwezo wa kujua mauzo akiwa na mashine hiyo ataweza kujua bidhaa zilizotoka, aliyetoa, muda ilipotoka na kiasi kilichobaki kupitia simu ya mkononi popote atakapokuwepo.

Amesema kazi nyingine ya mashine hiyo ni kufanya mauzo ya E-money kwa huduma za Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money kulipa mishahara pamoja na kuuza na kununua Luku, vocha aina zote za mitandao ya simu, Startimes, Zuku, Dstv na Azam Tv.

Amesema pia hurahisisha muda wa kusubiri huduma ambapo ukinunua luku kupitia mashine hizo huingia moja kwa moja kwenye mita badala ya kusubiri namba kutoka Tanesco au kwenye Dstv ambapo vocha huingia moja kwa moja.

Mbali na hizo pia mfanyabiashara hunufaika na Kamisheni inayotokana na kila huduma iliyofanywa na mashine pia mhusika kupata taarifa za mauzo na manunuzi ndani ya sekunde tano kila inapohitajika.

Meneja huyo amesema mashine hizo huuzwa kwa bei nafuu tofauti na mashine zingine ambapo hiyo huuzwa shilingi Laki 4(400,000/=) kwa mashine na kwamba ikiharibika mteja hubadilishiwa nyingine papo hapo au biashara ikifa mteja anarudishiwa fedha zake alizonunulia mashine.

Aidha amesema nafasi zinatolewa kwa anayehitaji kuwa wakala wa kusambaza mashine hizo  kwa kufika ofisini kwao zilizopo  kwenye Jengo la CRDB Karume Road au simu namba 0718 470499,0689 089422.

Pia kampuni hiyo inatangaza nafasi za kazi za kuuza mashine mbali mbali ambapo nafasi 10  kwa wenye fani za mauzo(sales) na nafasi 5 za IT.

Kwa sasa wanapatikana katika viwanja vya maonesho ya wakulima nanenane Mbeya kwenye banda la TASO .......

Nyote mnakaribishwa.

1 comment:

geoffrey mutalemwa said...

Mwezi Des, Simon& Felix waliniuzia ezeemoney machine ambapo waliahidi kuwa kuanzia trh Mosi Jan.2015 huduma ya Tigo Pesa na line kuunganishwa moja kwa moja na internet hadi leo bado nifanyeje nawao hawana majibu!