Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 4, 2014

SHEREHE YA KITCHEN PARTY YA NEEMA YA MWANGWALA YAFANA KATIKA UKUMBI WA JM MOTEL FOREST MPYA JIJINI MBEYA

 Neema Mwangwala ambaye ndiye anayefanyiwa Sherehe ya Kitchen Party akiwa na Furaha ukumbini wakati Sherehe ikiendelea.
Kwa hakika ilikuwa ni Bomba sana, hapa magari kibao yakiwa katika Msafara kuelekea katika Ukumbi wa JM Motel uliopo maeneo ya Forest Mpya
 Neema Mwangwala wa katikati akiwa na wapambe wake katika Sherehe yake ya Kitchen party
 Neema Mwangwala akiwa katika Picha ya pamoja na dada zake pamoja na Rafiki zake
 Neema Mwangwala akiwa anasalimiana na Mzaa Chema mama yake Mzazi na Kumshukuru katika Sherehe yake ya Kitchen Party.
 Neema Mwangwala kwa Heshima kubwa huku akiwa amepiga magoti akiwa anatoa neno la Shukurani kwa maneno aliyopewa na ambayo yatakuwa ya msingi katika Kujenga Familia yake.
 Mwenyekiti Kamati ya Mapambo Helieth akiwa anatoa neno kwa Neema Mwangwala wakati wa Sherehe yake ya Kitchen Party.
 Kwa mwendo  huu hapa wapiga picha kazi watakuwa nayo maana kila mtu mpiga picha, Mambo ya Sefie, mambo ya Whatsapp, Instagram , Facebook, Twitter yamehusika sana hapa .. ukodak wa Nguvu twende kazi.Neema Mwangwala akimlisha Keki mama yake Mpenzi kwa ishara ya upendo 
Mama Mzazi wa Neema Mwangwala akimlisha keki Binti yake mpendwa kwa ishara ya upendo na kumtakia Maisha Marefu na afya njema.
Sherehe akiwa inaendelea watu wakiwa wanapata Ukodak wa Nguvu 
Muda wa Chakula.. Neema Mwangwala akiwaongoza wageni waalikwa katika kupata Chakula wakati wa sherehe yake ya Kitchen Party
Sasa Muda wa sikelewuu... Ngololo.... Kwaito burudani zaidi .. kila mtu na Style yake wakati wa Sherehe za Kumfanyia Kitchen Party Neema Mwangwala
Wageni Mbalimbali wakiwa katika Kitchen Party Hiyo
One.. Two ... Three .. Four Twendee... hapa si mchezo... full kila mtu na style yake huku Neema Mwangwala nae akiwa hayupo nyuma kushirikikiana na wenzake kusherekea
Neema Mwangwala akiwa na pamoja na Kamati Nzito kabisa ya Maandalizi ya Kitchen Party yake akitoa salam za Shukurani za Dhati kwa wao kufanikisha Sherehe nzima mwanzo mpaka mwisho, vile vile akiendelea kuwashukuru wale wote walioungana nae katika Sherehe yake .

Picha zote na Mbeya yetu Blog.

No comments: