Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 6, 2014

MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ATEMBELEA BANDA LA NMB KATIKA MAONESHO YA NANE NANE NA KUFURAHISHWA NA HUDUMA BORA.

 Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi akiwa katika Banda la NMB kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayofanyika na huduma bora za Benki ya NMB
 Meneja wa Huduma kwa Wateja kutoka Benki ya NMB Happiness John Pimma wa kwanza kulia akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi wa kwanza kushoto juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo ikiwa ni pamoja na Huduma ya Internet Banking ambapo mteja anaweza kupata huduma kupitia Mtandao 'Internet' Masaa 24, Pia huduma ya kubadilisha Fedha za kigeni kwa Gharama nafuu zaidi mwisho ailielezea huduma ya NMB Chapchap ambapo mteja anaweza kupata kadi yake ya Benki ya NMB hapo hapo kwa Kiasi cha Shilingi Elfu kumi tuu.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbalizi Road ambaye pia ndiye msimamizi wa Banda la Benki ya NMB Katika viwanja vya nane nane Mbeya akiwa anamsikiliza kwa makini  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi  ambaye hayupo pichani
 Alex Masawe wa kwanza Kushoto akielezea Juu ya Mikopo mbalimbali ambayo inatolewa na Benki ya NMB  kwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi  wa kwanza Kulia ikiwa ni Mkopo kwa Bajaji, Boda Boda, Kilimo, wafanyakazi pamoja na wastaafu kwa uchache, pia alifafanua kwa kina jinsi ya Mikopo hiyo inavyoweza kupatikana.
 Lyambilo Kutoka Benki ya NMB akieleza kwa kina juu ya huduma bora ya Benki ya NMB ya Jihudumie kwa  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi wa kwanza Kulia   ambapo Mteja anakuwa hana haja tena ya kwenda Benki kila wakati lakini kwa kutumia ya Hudumie mfano mteja kuchukua pesa kupitia ATM, Mteja kupata huduma kupitia simu yake ya Kiganjani, pia kupata huduma kupitia kwa njia ya mtandao 'Internet'
  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi wa kwanza kushoto akipata maelezo ya kina kutoka kwa Rodgers Shipela wa kwanza kutoka kulia juu ya huduma ya NMB Foundation ambayo inahusika na kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima, wajasiliamali wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na Huduma zengine mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NMB
  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi  akipita katika Banda la Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB
  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi  wa kwanza kulia akiuliza baadhi ya wajasiliamali waliofika katika banda la mafunzo la Benki ya NMB kama wanapata mafunzo sahihi na ambayo endelevu, na kupata majibu kwa wanaofundishwa kuwa wanapata Huduma Bora na mafunzo yote ni endelevu kwao na yanawakuza zaidi kibiashara
 Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mh. Estalina Kilasi wa kwanza kushoto akipata maelezo ya kina juu ya Mkopo wa Pikipiki na Bajaji 
 Emanuel Mwambona wa kwanza kutoka kulia akiendelea kumuhudumia mmoja ya wateja ambaye alifika katika banda hilo wa kwanza kutoka kushoto wa pili kutoka kushoto ni Bi. Magoma kutoka Benki ya NMB
 Kutoka kulia ni Beatrice Mbawala , Josephat Mwalongo, Daniel Adam na Baraka Mwakyolile wote kutoka Benki ya NMB wakiwa wanatoa Huduma za ufunguaji wa Akaunti ya NMB Chap chap.
 Banda la NMB Katika viwanja vya nane nane Mbeya

Picha na Mbeya yetu


No comments: