Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 1, 2014

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WANATARAJIA KUFANYA ZIARA NCHINI MALAWI.

Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya safari hiyo iliyofanyika juzi kwenye Hotel ya Mbeya Peak, Mwenyekiti wa Kamati ya safari hiyo, Ulimboka Mwakilili ambaye pia ni Raisi Mstaafu wa UTPC alisema safari hiyo itaanza Agost 17, mwaka huu.

Baadhi ya waadhishi wa habari mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Mwenyekiti huyo

Add caption



BAADHI ya Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wanatarajia kufanya ziara (Study Tour) Nchi jirani ya Malawi kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali.

Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya safari hiyo iliyofanyika juzi kwenye Hotel ya Mbeya Peak, Mwenyekiti wa Kamati ya safari hiyo, Ulimboka Mwakilili ambaye pia ni Raisi Mstaafu wa UTPC alisema safari hiyo itaanza Agost 17, mwaka huu.

Alisema kutokana na urefu wa safari hiyo ambayo haimlazimishi mtu, kila anaevutiwa anapaswa kuchangia gharama za usafiri pamoja na chakula na malazi.

Alisema kima cha chini ni shilingi Laki mbili (200,000/=) kwa kila mtu mchango ambao mwisho wa kupokelewautakuwa Agost 8, mwaka huu.

Alisema safari hiyo ni muhimu kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya kutokana na manufaa ya kukutana na kujua mazingira ya kazi ya waandishi wa Habari wan chi jirani ya Malawi ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mema.

Aliongeza kuwa wanahabari hao wakiwa Nchini Malawi watafanya shughuli mbali mbali ambazo hakuzitaja kwa kile alichodai ratiba maalumu inapangwa kwa ushirikiano na wenyeji ambao ni waandishi wa habari nchini Malawi.

Kwa upande wake Mratibu wa Safari hiyo, Venance Matinya, alisema ni vema ikaeleweka kuwa safari hiyo haiwahusu Wananchama wa Klabu ya waandishi Mkoa wa Mbeya(mbeya press club) bali ni kwa mwandishi yeyote aliyetayari.

Alisema safari hiyo imeasisiwa na waandishi wa habari wakongwe hapa nchini na Mkoa wa Mbeya na waliowahi kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi kwenye Klabu.

Mwisho.

Na Mbeya yetu


No comments: