Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, July 18, 2014

TANESCO MBEYA YAPATA MAFANIKIO KUTOKANA NA USHIRIKIANO NA TLCO

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maganga, katika mkutano wa wanachama wa Chama cha Wakandarasi wazawa(TLCO) na Watumishi wa Tanesco uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden 
Add caption

SHIRIKA la Umeme (Tanesco)Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwaunganishia umeme wateja zaidi ya 20000 kwa kipindi cha miezi 12 ikiwa ni juhudi za kufikisha asilimia 35 ya watanzania kupata huduma hiyo.

Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maganga, katika mkutano wa wanachama wa Chama cha Wakandarasi wazawa(TLCO) na Watumishi wa Tanesco uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden jijini hapa.

Maganga alisema Serikali iliweka mikakati ili kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2015 asilimia 35 ya Watanzania wawe wanauwezo wa kupata huduma ya umeme bila vikwazo hali iliyosababisha Shirika hilo kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia malengo hayo.

Alisema mafanikio hayo ni kutokana na Shirika la Umeme kufanya kazi kwa ukaribu na Wakandarasi wa Mkoa wa Mbeya ambao wamewezesha kufanya vizuri tofauti na mikoa mingine licha ya kuwepo kwa changamoto chache ambazo alidai kuwa zinarekebishika.

Awali katika Mkutano huo, Chama cha Wakandarasi (TLCO) kupitia kwa Raisi wake, Kura Mayuma, waliwatupia lawama watumishi wa shirika la Tanesco Mkoa wa Mbeya kwa kuwabagua wakandarasi, kutoa lugha chafu dhidi yao na hata kuwaita vishoka pindi wanapoonekana katika ofisi za Tanesco kupata huduma.

Mayuma alisema mbali na watumishi hao kuwaita wakandarasi vishoka lakini pia kuna baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na kazi za ukandarasi na kumiliki makampuni binafsi na kujipatia kazi huku wakiwaacha wenye fani wakisota bila kazi licha ya kulipia leseni na ada za ukandarasi.

Na Mbeya yetuNo comments: