Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 17, 2014

MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA MKOA WA MBEYA WAFANYIKA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Mbeya, alisema wafanyabiashara ndiyo wanapaswa kufuata taratibu na sheria za manunuzi na Halmashauri ili kuepuka malumbano yasiyokuwa ya kawaida.

 Makamu wa Raisi wa TCCIA Taifa, Julius Kaijage, akiongea na waandishi wa habari


 SERIKALI imetakiwa kutunga sheria itakayosimamia sera ya uwekezaji na uwezeshaji ili iweze kutekelezeka kwa vitendo pamoja na kutoa adhabu kwa watumishi watakaoonekana kufanya vibaya.

Wito huo ulitolewa jana na Makamu wa Raisi wa TCCIA Taifa, Julius Kaijage, alipokuwa akichangia mada katika mkutano wa baraza la biashara la Mkoa wa Mbeya lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya.

Kaijage alisema suala la uwezeshaji na uwekezaji linatakiwa kupewa kipaumbele kwa kutungia sheria ili sera iliyowekwa na Serikali iweze klutekelezeka kwa vitendo na kutoa adhabu kali kwa wanaojaribu kukwamisha.

Alisema sekta binafsi ndiyo zinazoibeba serikali katika dhana ya uwekezaji hivyo ni vema watawala wakaacha kufanya kazi kimazoea bali wawe na mipango mkakati inayotekelezeka ili kuifanya sekta ya uwekezaji kuwa hai ikishirikisha sekta binafsi kwa mapana zaidi.

Aidha alizitupia lawama baadhi ya Halmashauri nchini kuendelea kukwamisha uwekezaji kwa kushindwa kuwa na utaratibu mzuri wa kuwalipa wazabuni wanaosambaza huduma mbali mbali katika ofisi zao.

Alisema Halmashauri hazina kumbukumbu za kutosha za wazabuni wanawadai na waliowalipa hali inayosababisha wengi kukimbia kutokana na mfumo mbovu unaotumika kutokuwa rafiki kwa mzabuni ambaye amewekeza katika kufanya kazi na Halmashauri.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Mbeya, alisema wafanyabiashara ndiyo wanapaswa kufuata taratibu na sheria za manunuzi na Halmashauri ili kuepuka malumbano yasiyokuwa ya kawaida.

Alisema wafanyabiashara wengi hufanya biashara na Halmashauri kwa mazoea bila kufuata taratibu na Sheria za manunuzi ambapo Mkuu wa idara anatoa maagizo ya kusambaziwa bidhaa ili hali mhasibu hajui wala Mkurugenzi.

“Tunapozungumzia uwekezaji na uwezeshaji kwenye Halmashauri zetu, wafanyabiashara ndiyo wenye makosa kutokana na kufahamiana kwake na mkuu wa idara wanakubaliana pasipo kuweka kumbukumbu jambo linalokuja kuwa gumu wakati wa malipo” alisema Kandoro.

Na Mbeya yetu

No comments: