Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 26, 2014

WANACHAMA WA YANGA MBEYA WAPEWA SOMO NA BENKI YA POSTA.

 Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Mbeya Humphrey Julius akiongea na viongozi wa matawi ya Yanga uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden uliopo jijini Mbeya wenye lengo la kuwahimisha kuwahamasisha mashabiki wao kufungua hizo akaunti.

WANACHAMA wa Klabu ya Yanga wakimsikiliza Meneja wa Benki ya Posta



Baadhi ya watumishi wa benki ya posta

Meneja wa Benki Mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius,
akiwaonyesha mfano wakadi watakayotumia katika benki hiyo 
Wanachama wa Yanga wakijaza fomu za kujiunga na benki hiyo





WANACHAMA wa Klabu ya Yanga wamehamasishwa kufungua akaunti katika Benki ya Posta ili kuchangia timu yao na kulipa ada bila usumbufu.

Hayo yalisemwa jana  katika Mkutano wa Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Mbeya na viongozi wa Matawi uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden uliopo jijini Mbeya wenye lengo la kuwahimisha kuwahamasisha mashabiki wao kufungua hizo akaunti.

Meneja wa Benki hiyo Mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius, alisema mradi huo ni mpya ambao utamwezesha mwanachama kuchangia klabu kila anapotumia huduma ya benki.

Alisema Benki ya Posta iligundua kuwa Klabu za Simba na Yanga zinawapenzi wengi ambao hawajui jinsi ya kuchangia timu zao ambapo ilibuni akaunti maalumu ambayo shabiki atapewa kadi itakayotumika kupata huduma za kifedha kama kawaida ambapo mchango wake huingia moja kwa moja kwenye klabu.

Alisema mwanachama na mpenzi wa klabu hiyo atakuwa akikatwa shilingi 250 kwa wiki kwenye akaunti yake ambazo zitakuwa zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti ya klabu hivyo kuzinufaisha na kumfanya mwanachama kuwa hai.

Alisema utaratibu huo utasaidia klabu kuacha utegemezi wa kuomba misaada kwa wafadhili na watu wasiokuwa na mapenzi na tumi bali itakuwa inapata michango na ada kutoka kwa wanachama wao moja kwa moja.

Nao baadhi ya Wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga Mkoa wa Mbeya wameulalamikia uongozi wa juu wa timu hiyo kwa kushindwa kutoa elimu kwa wanachama wake kuhusu mkataba walioingia na Benki ya Posta (TPB).

Wanachama hao ambao ni viongozi wa matawi ya Yanga Mkoa wa Mbeya ambao hawakutaka majina yao kuandikwa walisema kinachofanyika ni benki kufanya biashara kwa kuwahamasisha kufungua akaunti bila kuwaambia manufaa anayopata mtu mmoja mmoja.

Walisema utaratibu uliokuwepo awali ulikuwa kila mwanachama anachangia shilingi 1000 kwa mwezi ambapo kulikuwa na akaunti maalumu ya Benki ambayo kila mwanachama na mpenzi wa klabu alikuwa analipia huko.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: