Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, June 8, 2014

MBEYA CITY VETERAN CLUB YATOA MSAADA KWA YATIMA NA WALEMAVU JIJINI MBEYA.

Mwenyekiti wa klabu Veteran  Shaban Robert  wakipeana mikono ya shukrani na  Mkurugenzi wa kituo cha Child Support Tanzania, Noela Msuya,  mara baada ya kukabidhiwa misaada 

Baadhi ya wanachama wa Club ya Veterani wakiwa pamoja na watoto wa kituo cha Chirld Support


 Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango akiwashukuru Mbeya Veteran kwa kuguswa na namna kituo hicho kinavyojiendesha na kuamua kutoa msaada utakaowasaidia watoto kuendelea kuishi na kufurahia maisha kama watoto wengine walioko majumbani.

Mwenyekiti wa klabu Veteran  Shaban Robert akimkabidhi misaada kwa  Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango  
KLABU ya Mbeya City Veteran ambayo inajumuisha wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani imetembelea vituo viwili vya kulelea watoto yatima na kutoa msaada wa vitu mbali mbali.

Katika Ziara hiyo klabu hiyo iliyofanyika jana  ilitembelea vituo viwili vya Child Support Tanzania kilichopo Block T Soweto jijini Mbeya na kituo cha Nuru Orphans Centre kilichopo Uyole ambavyo vilipata msaada wa vitu mbali mbali.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Shaban Robert, alivitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na Sukari, Sabuni za mche, sabuni za unga, Vyandarua, Mafuta ya kupikia, dawa za meno na juisi vilivyogawiwa kwa vituo vyote viwili vikiwa na thamani ya shilingi Laki tatu.

Aidha alitoa wito kwa Taasisi, Asasi za kiserikali na binafsi zimetakiwa kuwa na utamaduni wa kutembelea vituo vya kulelea watoto yatima ili kujua changamoto wanazokumbana nazo kwa lengo la kuvisaidia.

Robert alisema suala la kulea watoto yatima si jukumu la mwenye kituo bali ni kila mtu mwenye utu wema kwa kuwa hao watoto hawakupenda kuwa yatima ama kuishi kwenye mazingira magumu.

Alisema endapo kila taasisi ama kundi la watu kama walivyo Mbeya Veteran wakajenga utamaduni wa kutembelea vituo hivyo ni rahisi kujua changamoto zinazovikabili na kusaidia kuzitatua jambo ambalo litamrahisishia mmiliki wa kituo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Child Support Tanzania, Noela Msuya, ambaye kituo chake kinahudumia watoto wenye ulemavu mbali mbali alishukuru kupata msaada huo kuwa utasaidia kuendesha kituo.

Alisema mbali na watoto hao kulelewa kituoni hapo kwa muda wa mchana na kisha jioni kurejeshwa makwao lakini hufundishwa masomo ya awali ukiwemo ufundi, uchoraji na sanaa kwa ujumla.

Naye Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango aliwashukuru Mbeya Veteran kwa kuguswa na namna kituo hicho kinavyojiendesha na kuamua kutoa msaada utakaowasaidia watoto kuendelea kuishi na kufurahia maisha kama watoto wengine walioko majumbani.

Alisema kituo chake kinalea watoto wasiokuwa na wazazi kabisa ambao asilimia kubwa huokotwa kwenye majalala au kutelekezwa na wazazi wao hivyo kituo kinakabiliana na changamoto za kuwalea kisha kuwapeleka shule umri unapokuwa umekaribia.

Alisema mbali na changamoto hiyo pia Serikali ambayo ndiyo huwapeleka watoto hao kituoni hapo kupitia Jeshi la Polisi na Ustawi wa jamii lakini hakuna msaada wowote anaoupata kutoka Serikalini.

Aliongeza kuwa kwa sasa kituo chake kinakabiliana na ukosefu wa uzio ili kudhibiti wizi wa vifaa vya watoto ambapo alitoa wito kwa taasisi na asasi mbali mbali kujitolea kuwajengea ukuta huo.

Mwisho.

Na Mbeya yetuNo comments: