Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 11, 2014

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AWATAKA MADEREVA NA WAMILIKI WA DALALDALA KUACHA MGOMO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akiongea na Madereva na wamiliki wa daladala jijini mbeya

Mwenyekiti wa Daladala Kanda ya Uyole Sunday Mwansasu amesema kuwa kitendo kilichofanywa na Halmashauri ya Jiji na Sumatra cha kuwapangia njia ambayo haiko katika mkataba wa leseni ya usafirishaji ni kitendo cha kuwaonea Madereva na Wamiliki wa magari kwani kwa ratiba hiyo hulazimika kutembea kilometa nne zaidi tofauti na njia ya awali.

Mchungaji William Mwamalanga akiwasii madereva wa dalala kutulia kumsikiliza kamada wa polisi wa mkoa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akitoka ukumbi wa mkutano mara baada ya kumaliza mazungumzo na madereza na wamiliki wa daladala


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amewomba Madereva na Wamiliki wa Daladala zinazofanya safari kati ya Uyole na Sokomatola  kuacha mgomo na kuendelea kutoa huduma ya usafiri wakati Mamlaka husika zikishughulika suala lao.

Kauli hiyo imekuja kufuatia mgomo wa siku mbili baada ya Daladala kugoma na kusitisha huduma za usafiri kwa kile walichodai kuburuzwa na Watumishi wa Halmashauri ya Jiji ,Polisi na Sumatra kwa kuwapangia njia ambayo imewasababishia umbali mreffu na kuongeza gharama za uendeshaji na kuwatia hasara kubwa.

Kamanda Msangi aliitoa kauli hiyo kufuatia kikao kilichoitshwa na Mlezi wa Daladala njia ya Uyole Mchungaji William Mwamalanga kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Tumaini uliopo Ilomba Jijini Mbeya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Madereva ambayo hayapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na Mamlaka hizo.

Msangi amesema kitendo cha kugoma kutoa ni kutesa wananchi ambao hawana hatia hivyo kuleta usumbufu usio wa lazima kwa Mamlaka husika zimepokea madai yao na kuahidi kuyafanyia kazi ndani ya siku mbili na kuyatolea maamuzi ambayo yataleta tija kwa pande zote.

Hata hivyo Kamanda alipokea malalamiko kutoka kwa madereva kuhusu Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani na kuahidi kuyafanyia kazi na hatasita kuchukua hatua endapo atabaini malalamiko yao yana msingi kama alivyochukua hatua hivi ya kuwafukuza Askari sita waliotuhumiwa kwa kupokea rushwa barabarani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Daladala Kanda ya Uyole Sunday Mwansasu amesema kuwa kitendo kilichofanywa na Halmashauri ya Jiji na Sumatra cha kuwapangia njia ambayo haiko katika mkataba wa leseni ya usafirishaji ni kitendo cha kuwaonea Madereva na Wamiliki wa magari kwani kwa ratiba hiyo hulazimika kutembea kilometa nne zaidi tofauti na njia ya awali.

Pia Mwansasu amelisema kuwa njia hizo haziwasadii hata abiria wenyewe kwani kwa safari ya kwenda mjini abiria wa Block T hupita Kabwe na anaporudi huachwa Soweto hivyo kutonufaika na ratiba hiyo na kulazimika kutembea kwa miguu au kutafuta usafiri mbadala.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu Madereva hao walikubaliana na Kamanda Msangi kwa kurejesha huduma wakati suala hilo likisubiri majibu ndani ya siku mbili kutoka Halmashauri ya Jiji na Sumatra ambao watakutana na Polisi wao kusimamia taratibu zitakazopangwa.

Madereva hao wlichukua fursa ya kumpongeza Kamanda wa Polisi kwa kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani ambavyo vilikuwa kero sugu na kuwafanya madereva kulichukia Jeshi la Polisi kutokana na utendaji mbovu wa baadhi ya Askari wa Jeshi hilo.

No comments: