Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 19, 2014

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAFANIKIWA KUMUUA JAMBAZI NA KUKAMATA BUNDUKI MOJA TUNDUMA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangiakionesha bunduki iliyokuwa na jambazi lililouwawa huko tunduma 




Hii ndiyo bunduki iliyokamatwa 


Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza RPC





MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE 19.06.2014.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 04:30 ALFAJIRI WALIONEKANA NA WALINZI WA USIKU WA ENEO LA SOKO KUU LA TUNDUMA LILILOPO KATIKA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI NA KUWATILIA MASHAKA KUWA WANA NIA YA KUFANYA UHALIFU YAANI UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.

WALINZI AMBAO WALIKUWEPO KATIKA ENEO HILO WALITOA TAARIFA KWA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA AMBAO WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO HILO. KUTOKANA NA TAARIFA HIZO MSAKO MKALI ULIANZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO.

MNAMO MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI YA LEO ASKARI POLISI WALIKUTANA NA WATU WAWILI WALIOWATILIA SHAKA KUTOKANA NA JINSI WALIVYOVAA KULINGANA NA MAELEKEZO YALIYOPEWA NA WALINZI. MMOJA KATI YA MAJAMBAZI HAYO ALIKUWA AMEVAA JAKETI KUBWA JEUSI NA MWINGINE AKIWA AMEBEBA MFUKO MKUBWA, WAKATI WAKIJARIBU KUWASIMAMISHA WATU HAO WALIANZA KUKIMBIA NA MMOJA KATI YAO ALIYEKUWA AMEVAA JAKETI ALIPOFIKA UMBALI WA MITA 20 ALITOA SILAHA BUNDUKI NA KUANZA KUFYATUA RISASI OVYO AKIELEKEA UELEKEO WA ASKARI.

BAADA YA KUONA HIVYO, ASKARI WALIJIBU NA KATIKA MAJIBIZANO HAYO YA  KURUSHIANA RISASI KATI YA MAJAMBAZI NA ASKARI POLISI, JAMBAZI MWENYE SILAHA ALIPIGWA RISASI UBAVUNI NA  KUFARIKI DUNIA, HIVYO KUFANIKIWA KUKAMATA  BUNDUKI MOJA AINA YA  AK- 47 YENYE NAMBA 592058 IKIWA NA RISASI 25 KWENYE MAGAZINE.

MTUHUMIWA MMOJA ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA MARA BAADA YA KUUPEKUA MWILI WA MAREHEMU KILIKUTWA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA CHENYE JINA JOSEPH THADEI KAPINGA, MKAZI WA MAFIGA, MOROGORO ALIYEZALIWA MKOA WA RUVUMA – SONGEA VIJIJINI TAREHE 07.09.1971.

KATIKA TUKIO HILO, HAKUNA MADHARA KWA WANANCHI/ASKARI YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA PAMOJA NA MTANDAO WAO WA UJAMBAZI.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SUZANE MHENDWA (45) MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAZARO KATENDE.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 KATIKA KITONGOJI CHA CCM, KIJIJI CHA UHAMILA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA WAKIWA NYUMBANI AMBAPO KIINI CHAKE KINACHUNGUZWA.

MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WANAFAMILIA KUTUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA KUTATUA MIGOGORO KATIKA FAMILIA HASA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA TATU:

WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954 AMH AINA YA  FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI, AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.  

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: