Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, June 24, 2014

HOT NEWS: HATIMAYE MTOTO ALIYEUNGANA SHINGO AFANYIWA UPASUAJI CCBRT. ANAENDELEA VIZURI

Mtoto Adorotea Emmanuel Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa anakabiliwa na majeraha ya moto na kusababisha ulemavu wa shingo amafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Dar es Salaam na sasa hali yake inaendelea vema.

Mtoto Adorotea Emmanuel Njavike akimwonyesha mwandishi wetu njinsi sasa anavyoweza kua mwenyewe kwa kupeleka mkono mdomoni mwake

Mama Milika ambae sasa amechangamka na kucheza mwenyewe
Mwandishi wetu Joseph Mwaisango akiwa amemshika mtoto huyo kabla ya kupata wadhamini wa kumsaidia

Wazazi wa mtoto Adorotea miezi mitatu iliyopita wakiwa uwanja wa ndege mbeya wakisubiria ndege kuelekea DSM kwa upasuaji wa mtoto huyo.




Mtoto Adorotea Emmanuel Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa anakabiliwa na majeraha ya moto na kusababisha ulemavu wa shingo amafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Dar es Salaam na sasa hali yake inaendelea vema.

Mama mzazi wa mtoto huyo Milika Kaberege(35) alisema kuwa mwanawe alipata majeraha hayo baada kuangukia motoni mwezi Octoba mwaka jana wilayani Njombe na kupatiwa matibabu Mbeya bila mafanikio.

Baada ya kuendelea kukosa matibabu yakinifu ndipoalionwa na vyombo mbalimbali vya habari na habari zake kuandikwa ndipo Bohari ya Madawa nchini MSD walipojitokeza kutoa usafiri wa ndege kutoka Mbeya kwa kushirikiana na Kikundi cha Wanawake ambaio walimfikisha CCBRT mwezi Machi mwaka huu.

Milika alisema kutokana na juhudi kubwa za Madaktari wa Hospitali hiyo mwanawe amefanyiwa upasuaji mara mbili na kwamba hali yake inaendelea vema na bado juhudi za Madaktari hao zinaendelea kurekebisha viungo vya mwanawe ikiwa ni pamoja na mikono yote miwili ilyopata majeraha.

Mama huyo ameshukuru Asasi mbalimbali zilizohangaikia matibabu ya mtoto wake wakiwemo waandishi wa habari wa Mbeya yetu ambao wamefuatilia maendeleo ya mtoto hata kufika Wodini kumjulia hali hivi karibuni na ameendelea kupata Faraja siku hadi siku kutoka kwa wadau wanaofika Hospitali.

Aidha amesema huenda mwanawe akatoka hivi karibuni baada ya kufanyiwa upasuaji wa mwisho wa mikono na haamini kwamba mwannae ambaya alikuwa akipata shida hata kula chakula na sasa anaweza kula na kutokana na juhudi kubwa za madaktari mtoto wake hivi sasa ameanza kutembea.

Mama Milika ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kuacha kuwaficha ndani bali wawapeleke Hospitali kama ya CCBRT ambao wanafanya kazi ngumu ya kurekebisha viungo na wagonjwa kurejea katika hali ya kawaida kutoa wito kwa wagonjwa kutokata tamaaa hali.

Upasuaji wa awali wa Adorotea ulifanyika Machi 21 mwaka huu wakati ule wa pili ulifanyika Mei 16 mwaka huu na upasuaji wa tatu utafanyika wakati wowote kuanzia sasa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa yeyote anayeguswa kutoa msaada wa hali na mali anaweza kumpatia kupitia simu yake ya mkononi namba 0753913472.

Na Mbeya yetu

No comments: