Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, May 21, 2014

UKAWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA MBEYA

Viongozi  wa ukawa wakiongea na waandishi wa Habari
 
Muungano wa Katiba ya wananchi (UKAWA) wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kesho kwenye viwanja vya shule ya msingi RuandaNzovwe jijini Mbeya.
 
Mkutano huo utahutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba,pamoja na viongozi wengine akiwepo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU)
 
Ukawa inaundwa na muungano wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chadema, Cuf pamoja na NCCR-Mageuzi ambao wamekuwa wakizunguka sehemu mbali mbali kuzungumzia katiba mpya na serikali tatu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija,katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peak, asema taratibu zote za mkutano huo zimekamilika.
 
Mwambigija amesema mbali na taratibu zote kukamilika lakini maandalizi yake yamekumbana na vikwazo vingi ikiwemo Jeshi la Polisi kukatalia kibali cha kufanya maandamano wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Lipumba.
 
Amesema mbali na kukataliwa kibali cha maandamano pia Halmashauri ya Jiji la Mbeya pia limekataa kupokea malipo kwa ajili ya gari la Matangazo(PA) jambo alilodai ni kuwanyima haki ya kikatiba ya kufanya maandamano pamoja na watendaji wa Serikali kuingiliwa na wanasiasa.
 
Amesema pamoja na changamoto hizo Mkutano utafanyika kama ilivyopangwa isipokuwa maandamano hayatakuwepo pamoja na wafuasi wao hawataruhusiwa kushika mabango ya aina yoyote ili kuepuka kuhujumiwa na upinzani wao ambao ni Chama cha Mapinduzi.
 
Ameongeza kuwa kukiwa na mabango CCM hupenyeza watu wake ambao hushika mabango ya kukashifu UKAWA pamoja na kupinga suala la serikali tatu katika mikutano yao kwa kuwavalisha sare za Chadema na UKAWA.
 
Amesema hali kama hizo zimeshajitokeza katika mikutano iliyofanyika Iringa na maeneo mengine ambapo baada ya kufanya uchunguzi wanabaini kuwa siyo wanachama wao bali ni mamluki waliopandikizwa kwa lengo la kutoa ujumbe tofauti na malengo.
 
Mwambigija amesema mtu yoyote atakayeonekana na bango la aina yoyote atapata cha moto kutoka kwa vijana wa Red briged ambao watakuwa wakilinda eneo la mkutano pamoja na kufanya doria usiku kucha kuangalia kama kuna dalili zozote za kuandaa mabango.

No comments: