Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 21, 2014

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI LAINGIA HATUA YA PILI LEO, KESHO WASHINDI KUPATIKANA

Kundi la Kwanza la Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili ya Mchujo katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents Mkoani Mbeya Wakipewa maelekezo kwaajili ya kuanza hatua ya mchujo leo.
 Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents Mkoani Mbeya kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika mazoezi mara baada ya kukabidhiwa Muswada (script) ikiwa ni hatua ya pili sasa ya shindano hili
 Ngoja tuangalie wenzetu wanafanyaje.....
 Wakitafakari muswada (script)..
Washiriki wakiendelea kuusoma Muswada (Script) kwa makini mara baada ya kukabidhiwa kwaajili ya hatua ya pili ya Shindano la Tanzania Movie Talents Mkoani Mbeya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya


Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya

Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wanatakiwa kupatikana kwaajili ya hatua ya tatu, washindi 30 watakaopatikana leo katika hatua hii ya pili wataendelea na hatua ya tatu ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatikana washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya nyanda za Juu Kusini na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=)
.
Mpaka sasa majaji wanaendelea kutafuta washiriki 30 watakaoendelea na shindano hilo kwa kanda ya nyanda za Juu Kusini na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya kanda ya nyanda za Juu Kusini katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=)

Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho katika kanda ya nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya na hatimaye kuhamia Kanda ya Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mtwara na wakazi wa Kanda ya Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.

No comments: