Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata
ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutupa
chooni kichanga jinsi ya kiume na kusababisha kifo chake.
Mwenyekiti
wa mtaa huo Juma Mbuza amesema walimtilia shaka mtuhumiwa Februari 18 mwaka huu
katika kilabu cha pombe za kienyeji baada ya kutoonekana na ujauzito,ndipo
walipomuulza kulikoni naye kudai kuwa amejifungua lakini mtoto yupo nyumbani.
Kauli hiyo
haikumridhisha Mwenyekiti huyo ndipo alipoamua kumtafuta balozi wake aitwae Daud
Dule na kumuuliza mtoto yupo wapi ndipo alipoanza kuwa na wasiwasi hali
iliyowalazimu kumkamata kutoa taarifa kituo cha Polisi Iyunga ambapo kabla ya
kufika Kituoni majira ya saa kumi na moja jioni mtuhumiwa alikiri kujifungua na
kutupa kichanga chooni Februari 18 mwaka huu.
Baada ya
taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha kati Febuari 19
ambapo Polisi hawakuweza kufika eneo la tukio licha ya Mwenyekiti wa mtaa
kufuatilia mara kwa mara kwa mkuu wa kituo cha Polisi Iyunga ambapo alijibiwa
kuwa watafika.
Hata hivyo
baada ya Polisi kutofika eneo la tukio kwa siku mbili tangu kukamatwa mtuhumiwa
Mwenyekiti wa mtaa alitoa taarifa katika kikao cha kata Februari 21 kufuatia tukio lililotukia
mtaani kwake na Polisi kushindwa kufika kwenye tukio siku tatu baada ya tukio
hali ambayo ilikuwa kero mtaani kwake.
Polisi
walifika eneo la tukio Februari 22 majira ya saa tano na nsu asubuhi
wakiambatana na Kikosi cha Zimamoto Jiji la Mbeya ndipo walipoanza anza kuibua
mwili wa mtoto ambapo ulikutwa umeharibika vibaya kutokana na kukaa kwa muda wa
siku nne bila kuibuliwa umbali wa kilometa saba tu kutoka Jijini.
Baada ya
mahojiano mtuhumiwa alidai sababu za kutupa kichanga hicho cha kiume ni
kutokana na kuogopa aibu kwa mumewe aliyepo Songea mkoani Ruvuma kikazi ambapo
mimba hiyo aliipata nje ya ndoa.
Uchunguzi
umebaini kuwa mwanamke huyo aliagizwa na mumewe kurejea Songea mwishoni mwa
mwaka jana lakini alikataa akidai kuwa angeenda mwaka huu baada ya kumsaidia
kaka yake shughuli za palizi.
Kabla ya
kichanga kilichotupwa chooni mtuhumiwa ana mtoto mwingine jinsi ya kike
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili na nusu.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Mtaa amelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kutoenda eneo la
tukio mapema hali ambayo inasababisha wananchi kujichukulia sheria mkononi hali
ambayo inweza kuepukika.
Baadhi ya
mashuhuda akiwemo mama Emilly Amnoni na Paulo Mbawala wamelaani vikali kitendo
kilichofanywa na mwanamke huyo kwani wamedai ni cha kinyama na ni cha kwanza
mtaani kwao hivyo wanaomba sheria iweze kuchukua mkondo wake ili kukomesha
kabisa vitendo vya kikatili Mkoani Mbeya.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment