Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, February 23, 2014

JAMII imetakiwa kuelewa kuwa madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la Boda boda ni salama tofauti na wanavyochukuliwa na baadhi ya watu wakiwaona kama wahuni na wenye kuleta uvunjifu wa amani.

Mkuu wa Miradi na utekelezaji wa Kampuni ya CitySign Promotion &  Marketing Agency Ltd ya Jijini Mbeya, Geophrey Mwangunguru,wakati akizungumza na madereva wa Pikipiki Jiji la Mbeya kuhusu maandalizi ya kuelekea kuanza kwa ligi ya Mpira wa Miguu kwa madereva wa Bodaboda katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya City pub.
Katikati Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo, Ibrahimu Mbembela alisema Kampuni yao kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Jiji la Mbeya(MUFA) wameandaa Sheria na taratibu mbali mbali za kuendesha ligi hiyo ambazo wamekubaliana na viongozi wa bodaboda.


Viongozi mbali mbali wa bodaboda wakiwa katika kikao hicho


JAMII imetakiwa kuelewa kuwa madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la Boda boda ni salama tofauti na wanavyochukuliwa na baadhi ya watu wakiwaona kama wahuni na wenye kuleta uvunjifu wa amani.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Miradi na utekelezaji wa Kampuni ya CitySign Promotion &  Marketing Agency Ltd ya Jijini Mbeya, Geophrey Mwangunguru,wakati akizungumza na madereva wa Pikipiki Jiji la Mbeya kuhusu maandalizi ya kuelekea kuanza kwa ligi ya Mpira wa Miguu kwa madereva wa Bodaboda katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya City pub.


Mwangunguru alisema lengo la kuandaa ligi kwa ajili ya madereva wa bodaboda ni kutaka kuifahamisha jamii kuwa nao ni sehemu yao na siyo waletaji wa vurugu kama wengine wanavyodhani  kupitia Mpira wa miguu utakaowakutanisha pamoja na wanajamii.


Alisema pia lengo la ligi hiyo na matarajio yao ni kuona Madereva wa boda boda Jiji la Mbeya linakuwa na timu bora na kubwa ambayo inaweza kushiriki michuano yoyote na wakati wowote ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya ikiwemo Ligi zinazoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF).


Aliongeza kuwa Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Aprili 27, Mwaka huu ikishirikisha timu 16 kutoka Kanda 7 za madereva wa Boda boda na kwamba viwanja vitakavyotumika ni pamoja na Uyole, Iyunga na Mwenge huku timu zitakazoingia Fainali kukipiga katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.


Aliongeza kuwa suala la zawadi bado linajadiliwa na kamati ya uendeshaji wa Ligi kutokana na mapendekezo mbali mbali ambapo Mshindi wa kwanza anaweza kujinyakulia Pikipiki Mpya yenye thamani ya Shilingi Milioni 2.2/=.


Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo, Ibrahimu Mbembela alisema Kampuni yao kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Jiji la Mbeya(MUFA) wameandaa Sheria na taratibu mbali mbali za kuendesha ligi hiyo ambazo wamekubaliana na viongozi wa bodaboda.


Alizitaja sheria hizo na taratibu kuwa ni pamoja na Usajilii wa wachezaji kuwa 30 ambapo kati yao wachezaji 20 ni madereva wa boda boda na 10 watatoka nje ya madereva.


Mchezaji haruhusiwi kuchezea timu zaidi ya moja, kikao cha maandalizi ya mechi husika kitafanyika kila siku asubuhi kabla ya mechi, mabadiliko ya wachezaji ni watano, mchezo ukivunjika utaendelea pale ulipoishia kutokana na taratibu husika kufuatwa.


Alizitaja sheria zingine kuwa ni kila timu kuwa na mpira mmoja ambao watakuwa nao kila mchezo, ada ya ushiriki wa mashindano ni Shilingi 30,000/=, timu ivae jezi yenye namba inayoonekana mgongoni, timu ikichelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi faini 10,000 na timu isipofika kabisa italipa shilingi 20,000/=.


Aidha aliongeza kuwa taratibu zingine ni kufuata sheria na kanuni za 17 za mpira wa miguu kama zinavyotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani(FIFA).

 Na Mbeya yetu No comments: