Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 27, 2014

MAAFISA Afya na Mifugo wametakiwa kutobweteka maofisini na kufanyia kazi kwenye makaratasi(Paper Work) badala yake wafanye kazi kwa vitendo

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Agnes Buchwa, alipokuwa akifungua kikao cha watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kuhusu Shughuli za Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba(TFDA) kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya uliopo Forest Mpya Jijini hapa.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa Chakula, Dawa, vipodozi na vifaa tiba(TFDA) Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Rodney Alananga,ambao ndiyo wandaaji wa mafunzo hayo alisema yamewalenga Maafisa afya, Mifugo, Famasia na wahasibu kutoka Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya.


MAAFISA Afya na Mifugo wakiwa katika semina hiyo
Picha ya pamoja


MAAFISA Afya na Mifugo wametakiwa kutobweteka maofisini na kufanyia kazi kwenye makaratasi(Paper Work) badala yake watumie taaluma yao kama walivyofundishwa mashuleni kwa kufanya kazi ya vitendo.

Mwito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Agnes Buchwa, alipokuwa akifungua kikao cha watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kuhusu Shughuli za Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba(TFDA) kilichofanyika leo katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya uliopo Forest Mpya Jijini hapa.

Buchwa alisema kuzagaa kwa uchafu katika maeneo mengi ya soko na mitaani ni kutokana na kutowajibika kwa maafisa afya na mifugo ambao ndiyo wenye lengo la kutembelea maeneo mbali mbali ili kujiridhisha na hali ya usafi wa maeneo na machinjio za mifugo lakini badala yake wanakaa maofisini na kuishia kuandika kwenye makaratasi.

Alisema hivi sasa TFDA inafanya kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Halmashauri kwa kuwatumia wataalamu wake ambao ni Maafisa Kilimo na afya kwa kufunga maeneo yaliyokithiri kwa uchafu ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kuwakumba wananchi kutokana na kutochukuliwa kwa hatua stahiki.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kukumbashana kila mtu wajibu wake ingawa kila mfanyakazi anaelewa lakini kinachofanyika ni kama matangazo ya biashara yanayojirudia rudia kila mara yakiwa na lengo la kumkumbusha mnunuaji ndivyo hivyo hata Serikali imeona ni vema watumishi wake wakapatiwa mafunzo kama hayo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa Chakula, Dawa, vipodozi na vifaa tiba(TFDA) Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Rodney Alananga,ambao ndiyo wandaaji wa mafunzo hayo alisema yamewalenga Maafisa afya, Mifugo, Famasia na wahasibu kutoka Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya.

Alananga alisema wameona ni vema kukumbushana Sheria za udhibiti wa chakula. Dawa vipodozi na vifaa tiba kutokana na kujitokeza kwa changamoto nyingi zinazosababishwa na utendaji wa kazi kila siku ili waweze kujadiliana na kukubailiana namna ya kukabiliana nazo kwa manufaa ya taifa.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya Halmashauri kushindwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo mbali mbali hali inayosababisha hatari kwa afya za binadamu ambapo pia Halmashauri hizo zimeshindwa kuunda Kamati za TFDA na kuzifanyia kazi.

Alisema changamoto nyingine ni pamoja na Halmashauri kushindwa kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za udhibiti licha ya kuelezwa katika Sheria na muongozo wa Tamisemi ambapo Halmashauri inapaswa kutenga Asilimia 40 ya makusanyo yaliyotokana na usajili na shughuli za TFDA na asilimia 60  kurudishwa makao makuu.

Aliongeza kuwa baadhi ya Halmashauri ambazo hutenga bajeti hiyo pia zinakabiliwa na changamoto ya kutotumia fedha hizo kama walivyoelekezwa na badala yake hutumia katika miradi mingine na kuacha kazi ya udhibiti kutokuwa na fedha hivyo kukwamisha kazi za wataalamu.

Alisema pia taarifa za utendaji kazi za wataalamu wa Udhibiti haziwasilishwi ofisini jambo ambalo linaashiria kazi hizo kutofanyika kama inavyotakiwa ambapo mtaalamu anatakiwa kuandaa ripoti kila anapofanya kazi na kupeleka ofisini ili kuona utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na Halmashauri kushindwa kupeleka asilimia 60 ya marejesho katika Mamlaka.

Hata hivyo katika mafunzo hayo wajumbe walijadili Majukumu ya udhibiti na mipaka ya ufanyaji kazi kati ya Mamlaka na Halmashauri ambapo Halmashauri zinapaswa kudhibiti utengenezaji, uingizaji, usambazaji usambazaji wa bidhaa mbali mbali na kukagua maeneo na bidhaa Sokoni.

Na Mbeya yetu

2 comments:

Anonymous said...

Safi sana Dr Agnes buchwa wanawake tunaweza

Anonymous said...

WAKIWEZESHWA