Katika ziara hiyo waziri alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara.
Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa shamba la
Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za Kijiji ili
kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu
kwa muda mrefu.
Rai hiyo
ameitoa alipofanya ziara katika shamba hilo ambalo liliuzwa hecta 7370 badala
ya 5500 ambazo ndizo zilizostahili na kuacha hecta 1870 ambazo ni eneo la
kijiji kabla ya kukabidhiwa shamba la NAFCO kabla ya kubinafsisha.
Ziara hiyo
imefanywa na Waziri ili kujiridhisha baada ya kupokea mgogoro huo kwa muda
mrefu bila majibu ya kuridhisha kutoka kwa watendaji wake hivyo kama Waziri
mwenye dhamana lazima atoe majawabu yenye uhakika badala ya kuolea majibu
ofisini.
Profesa
Tibaijuka alikutana na Uongozi wa Serikali ya kijiji kabla ya kukutana na
Mwekezaji na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika
kijiji cha Kapunga ambao pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Mbarali Matayo Mwangomo,Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kiffu na wataalam
mbalimbali kutoka wilayani na mkoani.
Waziri
Tibaijuka aliwashukuru wananchi wa Kapunga kwa uvumilivu wao kwani licha ya
mgogoro kudumu muda mrefu hawajafanya vurugu zozote hivyo alimtaka Mwenyekiti
wa kjiji hicho Ramadhan Nyoni kudumisha amani na upendo ili kumaliza mgogoro
huo bila uvunjifu wa sheria.
Profesa
Tibaijuka alipata maelekezo ya shamba hilo kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi,
Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza kuwa suala la
kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa majibu muda mfupi
ujao.
Hata hivyo
Bwana Vermaak alibainisha kuwa shamba hilo linakabiliwa na changamoto ya wizi
wa mbolea na mpunga kutoka kwa baadhi ya wananchi hivyo kuzorotesha uzalishaji
wa mpunga.
Aidha
Vermaak alimwambia Waziri kuwa kuharibiwa kwa miundo mbinu ya mifereji ya maji
kilometa 14 kutoka mto Ruaha kumepelekea kupungua kwa maji katika shamba hilo
hivyo kulazimika kulima chini ya kiwango.
Pia Bwana
Vermaak amemwambia Waziri kuwa wanalazimika kukodisha mashamba kutokana na
kuombwa na wananchi wa Kapunga ingawa hakuwa wazi juu ya mikataba ya ukodishaji
kuokana na mashamba hayo kukodishwa kwa shilingi 2,880,000 kwa plot na kutakiwa
kulipa mwekezaji tani 24 hadi 27 za mpunga baada ya mavuno.
Wananchi
wameonekana kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kauli iliyoungwa mkono na
Diwani wa Kata ya Itamboleo mheshimiwa Lwitiko Mwangosi ambaye amesema kuwa
licha ya kulipia shilingi 1,680,000 mwaka jana lakini hakupata kitu baada ya
mwekezaji kuchukukua mpunga wote aliovuna.
Baada ya
kukutana na uongozi wa kijiji na mwekezaji Waziri alihutubia wananchi na
kuwaambia kuwa hivi sasa mgogoro haupo baada ya kumwomba mwekezaji kuachia
hecta 1870 na kuwataka wananchi kuwa na subira kwani suala hilo halitachukua
muda mrefu na kama atakaidi basi taarifa ataiwasilisha kwa Rais kwani ndiye
mwenye dhamana ya kufuta hati miliki ya ardhi.
Katika
mkutano huo wanachi walipata fursa ya kuuliza maswali ambapo Emmanuel Kapalamba
alimwambia wazri kuwa vijana wamekosa ardhi ya kilimo hivyo kufanya maisha kuwa
magumu kiuchumina pia kwamba hawpati huduma za umeme na maji licha ya miundo
mbinu kupita katika kijiji chao.
Kwa upande
wa wanawake walimweleza waziri kuwa kijiji hakina zahanati kutokana na
iliyokuwapo kuporwa na mwekezaji hivyo kulazimika kutembea umbali wa kilomita
26 ili kupata huduma za afya katika hospitali ya Chimala.
Mkutano
ulifungwa kwa waziri kuchukua baadhi ya changamoto za maji,umeme na kilimo
kuzipeleka kwa mawaziri husika ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Katika ziara
hiyo wazir alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa na mwekezaji
ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana na soko ndani na nje
ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara ambapo baadhi ya hecta
hazijalimwa na nyingine kufanya majaribio ya zao la soya kinyume na mkastaba.
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment