Hii dimbwi ambalo maji yametuama na kutunza uchafu
Barabara iendayo kutokea uwanja wa zamani wa ndege mbeya ukiwa umejaa maji
Maji yakiwa yamezunguka stoo za wafanya biashara eneo la viwanda sido
Hapa kidogo ni afadhali kuliko maeneo mengine
Waendao kwa miguu pia ni shida kwani tope na maji ni shida kwao kwa kuwa wanapita kwa tabu sana
Hili eneo ndio krofi sana kwa kuwa hujaa sana maji na matope hivyo kusababisha magari kukwama kwa wingi na kuleta usumbufu.
Hapa ndio hapapitiki kabisaaaaaa,ni bwawa la samaki
Kwa mbali nafaka zikiwa zimetunzwa huku maji yakiwa yamezunguka eneo hilo
Barabara ikiwa tope tupuuu hivyo kufanya ushushaji wa nafaka kuwa mgumu
Hali ya barabara katika eneo la sido
mkoani Mbeya ni ya kutisha na kuhuzunisha sana.Eneo hilo ambalo
limetengwa maalumu na Jiji la mbeya kwa ajili ya stoo za wafanyabiashara
na pia ni maalumu kwa watu wanaohusika na ukoboaji,usagaji na kukamua
mafuta ya alizeti.Ukifika eneo hilo kipindi cha kiangazi huwa ni kavu
lakini kuna mashimo mengi yasiyorekebishwa.
Shida huwa inakuja kipindi cha masika na
mvua nyingi ambapo kupitika kwa maeneo yanayozunguka eneo hilo huwa ni
shida sana kwa waenda kwa miguu na pia magari makubwa na madogo
yanayoshusha na kupakia mizigo kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania.
Eneo hili pia ni kiungo muhimu sana kwa
wakazi wanaokaa maeneo ya uwanja wa ndege,kwa kuwa wengi wanatumia njia
hii kama ni shortcut ya kufika haraka majumbani mwao.Dj sek blog
ilifanya uchunguzi yakinifu kwa takribani wiki moja eneo hili na kuweza
kuvumbua mambo mengi sana,Moja ya mambo hayo ni kwamba kwa kiasi kikubwa
eneo hili hutumika kama makazi yasiyo rasmi kwa watoto wa mitaani,ambao
wengi hawana makazi au mahala pa kulala.
Watoto hao wa mitaani hutumia majengo
ambayo hayajamalizika vizuri kujiihifadhi kama makazi yao,Mtandao wetu
ulifanya mahojiano na baadhi ya wamiliki wa mashine na stoo za eneo hilo
kubwa ni kutaka kujua kwanini eneo hilo limetawaliwa na
madimbwi,mashimo makubwa na maji yaliyotuama kwa wingi.Wafanyabiashara
hao wameitupia lawama uongozi wa jiji kwa kushindwa kusimamia vizuri
eneo hilo ambalo limetengwa maalumu kwa ajili yao,wakiongeza kuwa
wanatoa kodi kila mwaka,kila mwezi walitegemea kodi zao zitatumika
kukarabati eneo hilo lakini kinyume chake imekuwa ni shida kwao.
Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa mgari
yanayokuja kushusha na kupakia yamekuwa yakipata sana shida kupita eneo
hilo hasa kipindi kama hiki cha mvua,hivyo wameiomba Serikali
kuwasaidia kukarabati eneo hilo.
Mtandao huuu ulijaribu kumtafuta mtu
anayeratibu na kusimamia eneo hilo lakini mpaka tunamaliza utafiti huu
hatukuweza kumpata.Rai ya mtandao wetu ni kwamba viongozi msikae tu huko
maofisini tokeni nje pia huku muone wanaicni wanavyokuwa na kero
nyingi.
No comments:
Post a Comment