Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 31, 2014

SHIRIKA la IMARISHA linalofadhiliwa na Watu wa Marekani limetoa msaada wa Vyombo vya kisasa kwa Kikundi cha Huduma Majumbani Mkoani Mbeya(KIHUMBE)

Mkurugenzi wa Mradi wa Imarisha na Kihukbe, Ptolemy Samweli, alisema walilazimika kuomba msaada wa vifaa hivyo baada ya kufanya utafiti kuhusu upatikanaji wa ajira za mafundi.




Baadhi ya wanafunzi wakiwa mafunzoni 



 Meneja mradi, Tuli Mtatiro 

Wakazi wa Sinde wakipata maelekezo toka kwa moja ya waalimu chuoni hapo






SHIRIKA la IMARISHA linalofadhiliwa na Watu wa Marekani limetoa msaada wa Vyombo vya kisasa kwa Kikundi cha Huduma Majumbani Mkoani Mbeya(KIHUMBE) wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 410 kwa lengo la kuendeleza fani ya ufundi kwa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Wakizungumza katika Hafla ya kuwatambulisha wakazi wa Eneo la Sinde A kuhusu umuhimu wa kuwatumia mafundi walijifunza na kujipatia uzoefu wa kutumia vifaa vya kisasa, Mkurugenzi wa Mradi wa Imarisha na Kihukbe, Ptolemy Samweli, na Meneja mradi, Tuli Mtatiro, walisema walilazimika kuomba msaada wa vifaa hivyo baada ya kufanya utafiti kuhusu upatikanaji wa ajira za mafundi.

Walisema kwa kusaidiana na shirika la Imarisha , Kihumbe iliona kuna tatizo la kwamba vijana wanaomaliza mafunzo ya ufundi hawapati ajira na kuamua kufanya utafiti ambao waligundua kwamba makampuni yenye magrreji na mafundi wa Cherehani wanahitaji watu wenye uzoefu wa angalau mwaka mmoja ndipo wanaweza kuwapatia ajira.

Walisema baada ya kugundua hivyo walifanya juhudi ya kuomba msaada wa vyombo vya kisasa kwa Imarisha ili kuweza kuwasaidia Vijana kupata uzoefu angalau wa Mwaka mmoja ili kuwarahisishia upatikanaji wa ajira.

Walisema Kihumbe imejikita zaidi katika kuwafundisha vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Nyanja za ufundi wa Magari na ushonaji ambapo hadi sasa kituo hicho kina wanafunzi 60, ambapo 30 wako katika ufundi wa magari na wengine 30 wakiwa katika ushonaji.

Kwa upande wake Mwalimu wa Fani ya ufundi wa Magari, Alpha Mhava alisema katika kitengo cha ufundi magari wamepokea mashine za kisasa zenye thamani ya Shilingi milioni 190 vyenye uwezo wa kufanya shighuli mbali mbali bila kutumia nguvu.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na Mashine ya kutolea matairi ya gari, mashine ya upepo, mashine ya kubalansia matairi, mashine ya kuangalia matatizo ya injini ya gari, mashine ya kuangalia mgandamizo wa injini ya Dizeli na Petroli, mashine za kuchomelea, kuchaji betri,kujazia upepona jeki za kubebea injini na kusombea.

Naye Mwalimu wa ufundi wa Ushonaji, Elezia Ngoya alisema wanalishukuru shirika la Imarisha kwa kuwaletea vifaa vya kisasa vya ushonaji vinavyotumia teknolojia ya kompyuta na umeme kwa madai kuwa vinaendana na mfumo uliopo wa sasa wa kutumia Digitali.

Alisema katika kitengo chake wamepokea vifaa zaidi ya 22 vyenye thamani ya shilingi Milioni 220  vikiwemo mashine za kushonea nguo za aina mbali mbali, Overlock(kumalizia ushonaji), kufuma mapindo, kushona mapambo mbali mbali, kutoboa matundu mbali mbali ya vifungo, Pasi ya umeme ya kisasa pamoja na mkasi wa umeme.

Na Mbeya yetu

No comments: