Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, January 20, 2014

Maandalizi ya Ligi ya mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda yameshika kasi ambapo waandaaji wa ligi hiyo wameanza kutekeleza ahadi yao kwa kuwaunganisha na mifuko ya jamii. Mbeya

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni Kampuni ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya Geophrey Mwangunguru katika kikao cha maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya alisema ligi hiyo itakuwa na timu 16 ambazo zitatoka katika kanda sita za bodaboda jijini Mbeya. 

Mratibu wa mashindano hayo Franklin Mwanjisi

mwakilishi wa Mfuko wa jamii wa PPF kanda ya Mbeya, Nyemo Chomola, alipokuwa akizungumza na viongozi wa vituo vya boda boda Jiji la Mbeya alipokuwa akiwahamasisha na kujiunga na mfuko huo katika mkutano ulioitishwa na Kampuni ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mpira wa miguu( Boda boda cup 2014).


Baadhi ya viongozi wa bodadada katika kikao hicho

Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji la Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.




 Maandalizi ya Ligi ya mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda yameshika kasi ambapo waandaaji wa ligi hiyo wameanza kutekeleza ahadi yao kwa kuwaunganisha na mifuko ya jamii.


Msemaji wa mfuko wa jamii wa PPF amewataka Madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda  kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kulingana na vipato vyao kwa manufaa ya maisha ya baadaye.

Mwito huo ulitolewa  na mwakilishi wa Mfuko wa jamii wa PPF kanda ya Mbeya, Nyemo Chomola, alipokuwa akizungumza na viongozi wa vituo vya boda boda Jiji la Mbeya alipokuwa akiwahamasisha na kujiunga na mfuko huo katika mkutano ulioitishwa na Kampuni ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mpira wa miguu( Boda boda cup 2014).


Nyemo alisema vijana wa boda boda wanaweza kunufaika na mfuko huo kwaajili ya maisha yao kutokana na mfuko huo kumlenga mjasiliamali yoyote kuhifadhi akiba zake kulingana na kipato chake.


Alisema mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PPF unawasaidia wanachama wake kutunza akiba zao kwa maisha ya baadaye ambapo mwanachama anauwezo wa kunufaika na mafao saba ambayo ni mafao ya uzeeni, kifo,ugonjwa, wategemezi, kujitoa,elimu na kiinua mgongo.

Alisema mafao hayo ni muhimu sana kwa madereva wa boda boda kwa kuwa wengi ni vijana na kazi wanayofanya ni hatari kutokana na kupata ajali nyingi za mara kwa mara hivyo kupitia mfuko huo unaweza kuwasaidia baada ya kupata matatizo kwa kunufaisha mwenyewe au wategemezi.

Awali wakijadili mfumo wa ligi hiyo mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Geophrey Mwangunguru katika kikao cha maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya alisema ligi hiyo itakuwa na timu 16 ambazo zitatoka katika kanda sita za bodaboda jijini Mbeya.

Alizitaja kanda hizo kuwa ni Kanda ya Sae, Kabwe, Iyunga na Uyole ambazo zitatoa timu 3 kila mmoja huku kanda ya Mafiati na Kadeghe zikitoa timo moja moja.


Mwaangungulu alisema lengo la kuandaa ligi hiyo ni kuwaunganisha madereva wa bodaboda ili kusudi waweze kutambuliwa na wanajamii  ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiwatuhumu kwamba ni wakorofi waliokosa ustarabu na umoja.

Alisema kupitia ligi hiyo wataweza kupata faida kubwa kwa kupatiwa elimu mbalimbali zikiwemo usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima,kuunganishwa na mifuko ya jamii, bima za afya,saccos na jinsi ya kujiwekea akiba.

Aliongeza kuwa ligi hiyo intarajiwa kuanza kulindima mapema mwezi wa nne baada taratibu zote kukamilika kwa kuzihusisha timu zaidi ya 16 za vituo vya bodaboda.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji la Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

 Aidha kwa upande wao viongozi wa boda boda wakiongozwa na Mwenyekiti wao Vicent Mwashoma na katibu Msumba Mdesa waliwapongeza waandaaji wa ligi hiyo kwa kuwakumbuka waendesha bodaboda na kuwahakikishia kushiriki ligi hiyo kwa amani na kwamba haina haja ya kulihusisha jeshi la polisi kwa madai kuwa wanauwezo wa kudhibitina wao wenyewe.

Na Mbeya yetu

No comments: