Huyu ndiye mwanafunzi aliyekuwa anatendewa ukatili huo |
Hii ndiyo ofisi ya mwalimu mkuu huyo ambayo ilikuwa inatumika kwa matendo machafu ya mwalimu huyo |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema atalifanyia kazi kutokana na kutokuwa Ofisini kwa wakati huo na kulitolea ufafanuzi unaotakiwa. |
Ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbeya |
MWANAFUNZI mmoja (Jina limehifadhiwa umri wake ni 16) wa
Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mkombozi iliyopo katika mji mdogo
Mbalizi Wilaya ya Mbeya Mkoani hapa ameshindwa kuendelea na masomo tangu shule
zifunguliwe akiogopa kuzomewa na wenzie baada ya kuhisiwa kulawitiwa na Mwalimu
Mkuu wake.
Hatua ya mwanafunzi huyo kushindwa
kufika shuleni kuungana na wenzie kumetokana na madai ya kuzagaa kwa tuhuma za
Mkuu wake wa shule kumwingilia kimwili mwanafunzi huyo mwenye jinsia ya kiume
wakati wa masomo ya jioni(Twisheni).
Akizungumza na waandishi wa habari
Mwanafunzi huyo alisema Mwalimu wake huyo ambaye alimtaja kwa jina la
Lusekelo Thom, kuwa anatabia ya kumbakiza yeye peke yake baada ya muda wa
masomo ya jioni kuisha na ndipo huenda naye ofisini na kuanza kumvua nguo.
Alisema tatizo hilo limedumu kwa kipindi
kirefu tangu Aprili Mwaka jana hadi Disemba 27, mwaka jana baada ya bibi
anayemlea kugundua (jina limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi) katika mahojiano
kutokana na mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani kila siku tofauti na
wengine.
Kwa mujibu wa majirani wa Mwanafunzi
huyo walisema kugundulika kwa maovu anayofanyiwa na mwalimu wake kulitokana na
upotevu wa fedha shilingi 20,000 na ndipo bibi huyo alipomuona mjukuu wake
akiwa na mkebe mpya na ndipo alipomuuliza kuhusu fedha zake ambapo Mwanafunzi
huyo alikataa kabisa.
Walisema baada ya kubanwa zaidi alidai
fedha za kununulia mkebe alipewa na Mwalimu wake na amekuwa na kawaida ya kumpa
fedha mwanafunzi huyo kila siku ikiwa ni pamoja na kumwambia asilipe ada ya
masomo ya jioni kwa madai kuwa atakuwa anamlipia.
Alipobanwa zaidi mwanafunzi huyo alidai
kuwa baada ya kupewa fedha na mwalimu huyo huenda naye ofisini na kufunga
mlango kisha huvua nguo zake na kumwamuru naye avue na kumlazimisha ashike
nyeti za mwalimu wake huku mwalimu naye akimshika shika na huo mchezo ulikuwa
ukifanyika kila siku na baada ya hapo mwalimu alikuwa akimrudisha mwanafunzi
kwa bibi yake majira ya saa mbili usiku.
Mashuhuda wa tukio hilo na baadhi ya
walinzi wa shule hiyo walikiri kuwepo kwa tuhuma za udharirishaji wa Mwalimu
huyo kwa Mwanafunzi kwa madai kuwa kila siku Mwalimu huyo kujifungia ofisini na
mwanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongozana naye kila mara.
Aidha baadhi ya ndugu walisema baada ya
kubaini hali hiyo walienda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha
Mbalizi ambapo Jeshi la Polisi lilimkamata Mwalimu huyo Januari 4, Mwaka huu na
kufanya naye mahojiano kisha kumpeleka mwanafunzi huyo Hospitalini kwa ajili ya
vipimo.
Hata hivyo Mwalimu huyo alipohojiwa
kuhusiana na tukio hilo alikataa kuhusika huku majibu ya vipimo vya Hospitali
vikionesha kutokuingiliwa kimwili kwa mwanafunzi ingawa Maelezo ya mtoto alidai
kuchezewa nyeti zake kila siku na kwamba suala la kuingiliwa kimwili alikuwa
akilazimishwa lakini hakuweza kufanikiwa.
Mwalimu huyo aliachiwa na jeshi la
Polisi katika kituo kidogo cha Mbalizi alipokuwa ameshikiliwa kwa ajili ya
mahojiano baada ya kuwekewa dhamana na Mratibu wa Elimu kata ya Utengule
Usongwe, Fredrick Silumbwe, na kwamba upelelezi bado unaendelea ili kubaini
kama kweli mwalimu huyo anafanya vitendo hivyo huku kukiwa na taarifa kuwa
Mwalimu huyo baada ya tukio hilo alisafiri na kuelekea Kibaha Mkoani Pwani
ambako yuko hadi sasa.
Kwa upande wake Mratibu Elimu kata
alipoulizwa kuhusiana na tuhuma dhidi ya mwalimu wake alisema hata yeye amekuwa
anazisikia mitaani na kuhusu kuweka dhamana alikiri kwa madai kuwa alipigiwa na
baadhi ya walimu na ndipo alipofanya hivyo kutokana na dhamana ni haki ya kila
mtu.
Naye Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya
Mbeya, Dionice Boay alipoulizwa kuhusiana na tuhuma za Mwalimu wake alikiri
kuzipata na kuongeza kuwa kutokana na Mwalimu huyo kufikishwa katika vyombo vya
Sheria wao kama Ofisi hawana cha kufanya zaidi ya kusubiri Ripoti ya Polisi
ambapo Mwalimu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
Alisema kama ofisi hatua ya kwanza ni
kumsimamisha kazi na kuteua Mwalimu mwingine kukaimu Ukuu wa Shule ya Msingi
Mkombozi wakati ofisi ikisubiri taratibu za Kimahakama kutokana na tatizo hilo
kuegemea kwenye makosa ya jinai.
Aliongeza kuwa Ofisi pia inatarajia
kufanya ukaguzi katika shule hiyo ili kubaini kama Mwalimu alikuwa na makosa
mengine na kujua sababu ya Mwanafunzi kutoenda shule hadi sasa licha ya wenzie
kuendelea na masomo.
Hata hivyo Kituo cha Haki za Binadamu
kilionesha mshangao kutokana na mtuhumiwa wa tukio hilo kuachiwa kwa dhamana
ili hali upelelezi haujakamilika na hakuna hatua zozote ambazo Jeshi la Polisi
linaonesha kulifanyia kazi ambapo mtuhumiwa alifikishwa Polisi Januari 4, Mwaka
huu.
Mwenyekiti wa Kituo cha Haki za Binadamu
Mkoa wa Mbeya, Said Madudu alisema Jeshi la Polisi limechukulia suala hili kama
ni siasa kwa kuchelewa kuchukua hatua kwa wakati huku mtoto akiendelea kukosa
haki yake ya msingi ya masomo.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema atalifanyia kazi
kutokana na kutokuwa Ofisini kwa wakati huo na kulitolea ufafanuzi unaotakiwa.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa umebaini
kuwepo kwa rushwa zinazopelekea upelelezi wa kesi hiyo kuchelewa kutokana na
kuwepo kwa taarifa za Mtuhumiwa kutoa fedha shilingi Milioni Tatu ambazo bado
haijulikani mgao wake uliwagusa akina nani.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment