Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 12, 2013

Wakazi wa jiji la mbeya wametakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la uhaba wa maji uliopo hivi sasa.

mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya Simion  aliongozana na madiwani wa kata ya IGANZO,Mh USWEGE FULIKA na diwani wa kata ya Mwansekwa GASPER NGONELA ambapo wameitaka mamlaka kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wanao zunguka vyanzo vya maji.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya Simion Shauri
Hii ndiyo hali halisi ya chanzo  cha mto sisimba





Wakazi wa jiji la mbeya wametakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la uhaba wa maji uliopo hivi sasa.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na mazingira jiji la mbeya SIMIONI SHAURI alipokuwa kwenye ziara yakukagua vyanzo vya maji vya IZIWA,NSOHO na  SISIMBA.

Aidha katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo amesema vyanzo hivyo kwa sasa vinatoa maji  kwa asilimia 87 ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo vilikuwa vikitoa asilimia 100

Akielezea sababu za mabadiliko hayo amesema yamechangiwa na uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuchoma moto vyanzo hivyo na kilimo holela.

Wakati huo huo mwana sheria wa Mamlaka ya Maji mkoani mbeya SIMONI BUKUKU amepeleka lawama kwenye sheria za misitu kwa kushindwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya miti gani inayofaa kupandwa karibu na vyanzo hivyo.

Katika ziara hiyo mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya aliongozana na madiwani wa kata ya IGANZO,Mh USWEGE FULIKA na diwani wa kata ya Mwansekwa GASPER NGONELA ambapo wameitaka mamlaka kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wanao zunguka vyanzo vya maji.

No comments: