Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 24, 2013

TUNATANGAZA UTALII WA NDANI: IFAHAMU HISTORIA YA ZIWA NYASA NA UNDANI WAKE.


Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.

Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.
 Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.

 Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
 Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
 Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
 Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
 Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
 Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa

 
 Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo ewa 


Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.

No comments: