Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 3, 2013

KITUO CHA CHILDREN SUPPORT TANZANIA CHA ADHIMISHA SIKU YA ULEMAVU DUNIANI. MBEYA

Mgeni rasmi toka benki ya NMB akikata utepe kuzindua uwanja wa michezo wa kituo hicho
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupokea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.
Mtoto Maxel mlemavu wa mikono na miguu nae akiwa katika vazi rasmi la mahafali ya kumaliza Darasa la awali kuingia darasa la kwanza




Kituo cha kulelea na kufundishia watoto cha Children Support Tanzania kilichopo Block T Jijini Mbeya kimeungana na Ulimwengu mzima katika kuadhimisha siku ya Ulemavu Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 3 Disemba kwa kuzindua uwanja wa mazoezi na mahafali ya Chekechea.

Aidha kituo hicho kimetumia siku hiyo kwa kusheherekea mahafali ya watoto 15 ambao wanavuka hatua kutoka Chekechea tayari kwa kujiunga na Darasa la Kwanza mwakani baada ya kupata sifa za kujua kusoma na kuandika.

Katika Sherehe hizo zilizofanyika katika Viwanja vya kituo hicho zilizohudhuriwa na wazazi wa wanafunzi wanaosoma hapo pia umezinduliwa uwanja wa mazoezi unaofahamika kwa jina la CST Fun Village ambao utakuwa na michezo mbali mbali ya watoto.

Akizungumza katika Sherehe hizo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupikea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.

Amesema kituo hicho kinapokea watoto wenye ulemavu wa akili, Viungo,viziwi, wanaoishi katika mazingira magumu na watoto wa kawaida ambapo wanafundishwa elimu maalumu ya darasani, ufundi, mziki na michezo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.

Amesema kauli mbiu ya Siku ya walemavu Duniani inasema, “Vunja vizuizi, fungua milango kwa jamii jumuishi kwa maendeleo kwa wote”ambayo inapaswa kuenziwa kwa kuwajengea mazingira ya kuwapenda walemavu na kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi.

Na Mbeya yetu



No comments: