Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape Nnauye akiwahutubia maelfu wa Wananchi wa Jiji la Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi RuandaNzovwe. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akisalimiana na Nape katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akijibu baadhi ya kero za Wananchi katika mkutano huo. |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amepozi baada ya kuvalishwa mavazi ya kichifu na wazee wa mila wa Mkoa wa Mbeya ambavyo ni Mkuki, mgolole na kigoda. |
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi wa Jiji la Mbeya katika Mkutano huo. |
Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa Mkoa wa Mbeya kupitia UVCCM, Nwaka Mwakisu akiwa amebebwa juu kwa juu na vijana kwa mchango wake mkubwa kwa vijana wa Mbeya |
Meza kuu wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio yanayoendelea jukwaani. |
Vijana wa Mwanjelwa wakiwa wamembeba msombesombe mlezi wao Mbunge wa Viti maalum Mary Mwanjelwa wakimpeleka kwenye gari lake baada ya kukamilika kwa mkutano. |
PICHA NA MBEYA YETU BLOG.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Taifa, Abdulrahman Kinana, ameonesha kukubalika kwa wananchi na Wakazi wa Jiji
la Mbeya baada ya yeye na ujumbe wake kupata mapokezi makubwa tofauti na
matarajio ya watu wengi kutokana na Jiji la Mbeya kuongozwa na Mbunge wa
Chadema.
Kinana aliyekuwa akiwahutubia maelfu ya
wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vya jirani katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ruandanzovwe Ilomba Jijini
Mbeya, aliwakonga watu waliofurika uwanjani hapo kutokana na kile alichokuwa
akiwahutubia kuwagusa hadi moyoni.
Kinana huku akishangiliwa na umati wa
wananchi bila kujali itikadi zao alisema Chama cha Mapinduzi hakina sababu ya
kujiita Nambariwani kutokana na kuwakandamiza wananchi wa hali ya chini na
kuishi maisha magumu kutokana na viongozi wa chama hicho ngazi ya juu kufanya
ndivyo sivyo.
Alisema Chama cha Mapinduzi ndicho
chenye Serikali hivyo kitendo cha kuuza viwanda kwa Wawekezaji ambao
wameshindwa kuviendeleza ni kuwakosesha fursa wananchi ya kufaidi matunda ya
nchi yao ambapo aliongeza kuwa kama Serikali iliona watu hao walishindwa
kuviendeleza viwanda hivyo ni bora wakapokonywa wakapewa watu wengine wanaweza
kufanya kazi ili watanzania wengi wapate ajira.
Aliongeza kuwa Katiba ya Nchi inasema
hakuna mtu aliyejuu ya mwingine zaidi ya Wananchi, hivyo viongozi wa Serikali
hususani Mawaziri hawana sababu ya kuwapangia wananchi kitu cha kufanya bali
wanatakiwa kuwauliza wanachotaka kufanyiwa ni nini kwa sababu wananchi ndiyo
wako juu ya viongozi.
Katika Mkutano huo Kinana alisimikwa
kuwa Mkazi wa Mbeya baada ya kuvalishwa Mgolole na kupewa Mkuki na kigoda na
viongozi wa kimila wa Mkoa wa Mbeya kama ishara ya kumkaribisha Mkoani hapa.
Wakati Mkutano ukimalizika uwanjani hapo
baadhi ya Vijana wa Mwanjelwa ambao walitaka kujiunga na chama cha mapinduzi na
kuomba kukabidhiwa kadi za chama hicho ambapo jukumu la kuwakabidhi aliachiwa
Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa (Mnec) Capt. Shitambala, waliwasifia walezi wao
kwa kuwaunganisha na chama pamoja na misaada mbali mbali.
Vijana hao walipotakiwa kusema lolote
mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye, walisema juhudi
za wao kuonekana na kusimama mbele ya jukwaa ni kutokana na elimu nzuri waliopewa
na walezi wao ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa Mkoa wa Mbeya
kupitia UVCCM, Nwaka Mwakisu na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary
Mwanjelwa.
Walisema walezi hao huwasaidia pindi
wakiwa na matatizo mbali mbali ya kiushauri na kifedha kwa kuwaunganisha pamoja
na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya vyama vya Siasa ambavyo huwatanguliza
mbele kwenye vurugu ili hali wao hubaki nyuma na kukimbia.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment